Mtindi unaorodheshwa
kuwa ni miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi
katika mwili wa mwanadamu .
Miongoni mwa
virutubisho vinavyopatikana katika maziwa ya mgando (mtindi) ni pamoja na
calcium, phosphorus, rhiboflavin (vitamin B12), potassium, iodine na
vinginevyo.
Asilimia kubwa ya
wanajamii wengi hupendelea kusindika kinywaji hiki kwa muda mrefu na kisha
kukitumia, hususani jamii ya Wamasai na Kimang’ati, ambao huyaweka maziwa hayo
kwenye kibuyu.
Mbali na kuwa
virutubisho hivyo vinapatikana ndani ya maziwa ya mgando ambayo wengi
tunayafahamu kama mtindi, pia hupatikana bakteria hai ambao ni muhimu kiafya
katika mwili wa binadamu (probiotics).
Watafiti wamebaini
kuwa bakteria wanaopatikana katika mtindi hurefusha maisha kwa wazee, ni kinga
kubwa kwa kina mama kutokana na maambukizo ya magonjwa ya ukeni na hata
hupelekea kupunguza kiwango kikubwa cha shinikizo la damu la juu
(high blood pressure level), lakini pia husaidia kupunguza uzito mkubwa na unene uliopitiliza.
Kama inavyojulikana, kiwango cha shinikizo la damu kikiwa juu huleta magonjwa
kama mshtuko wa moyo na kiharusi. Tafiti hizo zinasema kuwa probiotics
zinasaidia kudhibiti viwango vya insulin, lehemu na glukosi mwilini visizidi.
Wataalam hao kupitia
tafiti hizo wamesema kuwa maziwa
yamgando (mtindi) yameokoa maisha ya walio wengi baada ya tathimini kutoka kwa
wagonjwa zaidi ya 540 waliosumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu.
Pamoja na hayo, idadi
kubwa ya wagonjwa waliotumia kinywaji hiki walifanikiwa kupona baada ya muda
usiopungua wiki nane, hivyo inapendekezwa kutumia kinywaji hiki kama sehemu ya
lishe yetu.
No comments:
Post a Comment