Ama kwa hakika, ‘ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.’ Huko
Huaxi, nchini China, mtoto wa miaka miwili amefanyiwa upasuaji wa kutoa kifusi
mwilini mwake.
Hii ni baada ya madaktari kugundua kuwa kifusi hicho kilipaswa
kuwa pacha wake aliyeshindwa kukua ipasavyo.
Xiao Feng alipelekwa hospitali baada ya tumbo lake kuwa
kubwa kiasi cha kuwa alijikuta akishindwa kupumua.
Alipolazwa, madaktari walichukua picha za ‘X-ray’ na ‘MRI’ na kugundua kuwa Feng alikuwa amebeba mimba isiyokua na hivyo kuamua kumfanyia upasuaji.
Alipolazwa, madaktari walichukua picha za ‘X-ray’ na ‘MRI’ na kugundua kuwa Feng alikuwa amebeba mimba isiyokua na hivyo kuamua kumfanyia upasuaji.
Walikiondoa kifusi hicho changa kilichokuwa na ukubwa wa
inchi 10 na tayari kilikuwa kimeanza kuwa na uti wa mgongo na vidole. Mimba
hiyo ilitakiwa kuwa pacha wa mtoto huyo (yaani mmoja alikulia tumboni mwa
mwenzie). Pacha huyo wa sponji angekua na kuwa mtoto wa kiume.
Mapacha wanaofanana hutokea pale yai linapojigawa wakati wa
urutubishaji na mapacha walioungana hutokea pale yai linaposhindwa kujigawa
kikamilifu. Kwa kesi ya Feng, baada urutubishaji, yai lilishindwa kujigawa na
upande mmoja ukamezwa na upande wa pili.
MTOTO AMEZALIWA AKIWA NA MIKONO NA MIGUU MINNE
MTOTO
wa kiume wa maajabu amezaliwa akiwa na mikono minne na miguu minne jambo ambalo
liliwashangaza watu wengi pamoja na familia yake.
Mtoto
huyo kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa saa 3 katika
hospitali ya Mulago nchini Uganda.
Paul
Mukisa alizaliwa Septemba mwaka huu na mwanamke aitwaye Margaret Awino mwenye
umri wa miaka 28.
Mama
huyo baada ya kuona hali ya mtoto wake huyo kuwa ya kushangaza, alishirikiana
na familia yake na kuamua kumkimbiza hospitali iliyo karibu na kijiji chao cha
Nabigingo.
Baada
ya mtoto huyo hali kuendelea kubadilika, walimhamishia kwenye hospitali ya Mulago
iliyopo Kampala kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Baada
ya kufika hospitalini mtoto Paulo alifanyiwa upasuaji na kutolewa kiumbe kiingine
kwenye mwili wake chenye miguu miwili na mikono miwili lakini hakina kichwa
wala moyo. Iwapo kiumbe hiki hakingejiunganisha na mwili wa Paulo na kikue
vizuri, kingekuwa pach wa Paulo.
Dkt.
Nasser Kakembo aliyeshiriki kwenye upasuaji huo, alikiambia kituo cha runinga
cha CNN kwamba walitoa pia mbavu kutoka kwa kiumbe kilichoungana na mtoto huyo.
“Tulitoa mbavu zake za kulia na kushoto
zilizokuwa zimeungana, tulizuia damu na kuziba vidonda,”
alisema
Dkt. Nasser.
Wataalam
hao wa afya wanasema ni nadra sana mtoto kama huyo kuzaliwa ingawaje kuna uwezekano
mkubwa wa kuzaliwa mtoto kama huyo.
Ndiyo
maajabu hayo ya dunia, kile ambacho hufikiri kutokea katika dunia hii huwa
kinatokea katika hali yoyote muda wowote na mahali popote.
KIAZI CHAMEA NDANI YA KIZAZI
Hali ilipoanza
kubadilika, baada ya kulalamika kuhusu maumivu ya tumbo, aliamua kumuona daktari
na baada ya uchunguzi aligunduliwa kuwa ana kiazi ambacho kilikuwa kimeota mizizi
ambayo ilianza kumea ndani ya kizazi chake.
Kulingana na
gazeti la Nation nchini Kenya, msichana huyo amedai kuwa mamake alimshauri kwamba
iwapo angependelea kuzuia mimba basi alifaa kuweka kiazi ndani ya kizazi chake.
Licha ya hatari
aliyokumbana nayo mwanamke huyo hakuathirika huku kiazi hicho kikitolewa bila kufanyiwa
upasuaji.
MFAHAMU MTOTO MREFU DUNIANI
Ama kweli ya Mungu mengi. Huko nchini India msemo huu wa Waswahili
ulidhihirika baada ya kuzaliwa mtoto mwenye uzito wa kilo saba na urefu wa zaidi
ya futi mbili na kupewa jina la Karan Singh.
Baba wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 35 alisema kuwa, “wakati
anazaliwa, alikuwa na urefu na uzito usio wa kawaida. Tulifikiria kwamba huenda
akawa ana matatizo fulani ya kiafya. Lakini madaktari walituambia kuwa ni mzima
na mwenye afya tele.”
“Urefu na uzito wake uliwashtua madaktari, hatimaye kuingizwa
kwenye kitabu cha ‘Guinness Book of World Records’ ambapo anatambulika
kama mtoto aliyezaliwa mrefu zaidi na uzito mkubwa zaidi duniani kwa watoto
waliowahi kuzaliwa.
Cha kushangaza ni kwamba kwa sasa Karan ana umri wa miaka mitano
na urefu wa futi tano na inchi saba. Hii inamfanya kuwa mtoto mrefu zaidi
duniani kwa watoto walio na umri wa miaka mitano. Babake Karan ana urefu wa
futi sita na inchi saba huku mama yake Shweatlana Signh, wa umri wa miaka 26,
ni mrefu zaidi kwa kuwa na urefu wa futi saba na inchi tatu.
Kuna kipindi alitambulika kama mwanamke mrefu zaidi India na
kuendelea kufahamika kuwa ni miongoni mwa wanawake warefu zaidi kusini mwa
Asia.
Baba yake Sanjay aliongeza kuwa, “Sisi ni familia ya watu warefu.
Kama nikienda mahali fulani, najikuta kuwa ni mtu mrefu zaidi katika eneo hilo.
Lakini ninaporejea nyumbani ninakuwa mfupi ukinilinganisha na mke wangu.”
Naye Shweatlana alisema kuwa, “kila mwaka Karan anaongezeka futi
moja na inchi tano kila mwaka.” Hii ni kutokana na kuzidi kwa homoni za ukuaji.
Hata hivyo, mama yake alisema kuwa anapata wakati mgumu sana
kwenye kutafuta mavazi ambayo yatamtosha.
No comments:
Post a Comment