KLINIKI YAMPANDIKIZA MBEGU ZA MWANAUME MWINGINE
Nchini Marekani katika mji wa Commack, New York,
mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Nancy Andrew alipata ujauzito
usiotokana na mbegu za mumewe baada ya kupandikizwa mbegu za mwanaume mwengine katika
kliniki ya upandikizaji (New York Fertility Clinic).
Yeye na mume wake walitegemea kuongezeka kwa mtoto katika
familia yao. Walichokuwa hawatarajii ni kupata mtoto mweusi kuliko wazazi wake.
Vipimo vya kutambua vinasaba (DNA Test) vilionesha
kuwa madaktari katika kliniki ile walipandikiza mbegu za mwanaume mwengine
kwenye mayai ya Nancy Andrew.
Wapenzi hao mpaka sasa wanamlea mtoto huyo waliyempa
jina la Jessica kama wa kwao.
Hata hivyo, wawili hao wanaona hawakutendewa haki na
mwenye kiliniki hiyo pamoja na daktari aliyechanganya mbegu hizo.
Je, ilishawahi kukutokea hiyo?
Pia, tuambie kero au hali ya huduma za afya zikoje katika
hospitali iliyo karibu nawe. TABIBU itafika kuitatua kupitia 0656 269 215 (SMS
tu).
AMEPEWA MOYO NA MAPAFU YASIYOFAA NA KUFARIKI DUNIA
Mh! Kwa
kweli inasikitisha.
Huko
Marekani, msichana aliyefahamika kwa jina la Jésica Santillán, aliwasili katika hospitali ya Duke
University Medical Center kutokea nchini Mexico ili kupata matibabu kufuatia
kuwa na matatizo ya moyo na mapafu.
Jésica
alikuwa ni msichana wa umri wa miaka 17, raia wa Mexico, pengine alikuwa na
ndoto nyingi kwa taifa lake na familia kwa ujumla lakini alifariki dunia muda
mfupi mara baada ya kufanyiwa upasuaji.
Sababu ya
kifo chake ilitokana na kuhamishiwa moyo na mapafu (heart-lung transplant)
kutoka kwa mtu ambaye hafanani naye kundi la damu.
Je,
ulishawahi kupatwa na tatizo kama hilo au linalofanana na hilo?
Pia,
tuambie kero inayokusumbua katika zahanati au hospitali unayokwenda kupata
huduma ya matibabu na TABIBU itafika kuiondoa kupitia 0656 269 215 (tafadhali
tuma SMS tu).
No comments:
Post a Comment