EDSON: NAANDAA TAMASHA KUSAIDIA YATIMA
Na Kennedy Chaya
MSANII wa muziki wa Injili Edsoni Mwasabwite
anatarajia kuandaa tamasha la kusaidia yatima mwezi Novemba. Tamsha hilo pia
linatarajia kuwalenga wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze
kujiona kama sehemu muhimu katika jamii.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini
Dar es Salaam, Edson alisema ni kawaida yake kutoa shukrani na sadaka ya fungu
la kumi kusadia watu wasiojiweza.
Edsoni anasema, “nafahamu machungu wayapatayo
watoto yatima hivyo ni muhimu kuwafariji ili wasikate tamaa kwani ipo siku yao
watakapofanikiwa kama ilivyo kwangu na wengine.”
Aliongeza kuwa ni muhimu jamii kusamianiana,
kuheshimiana na kutambua kila mtu ana nafasi yake katika jamii, kwani masikini
wa leo ni tajiri wa kesho.
Edson amepata umaarufu sana kupitia albamu yake
ya kwanza ya ‘Ni Kwa Neema na Rehema’ na wimbo wenye jina hilo lililopendwa na
watu wengi. Wimbo huo umetawala katika matamasha na sherehe za harusi nyingi
hapa nchini.
Msanii huyo kwa sasa anaandaa video ya albamu
yake ya pili, yenye jina la ‘Mungu Amenisaidia’.
MZEE YUSUPH: MFALME WA TAARAFU ASIYE NA MPINZANI
Na Kennedy Chaya
NYOTA wa muziki wa Taarab, Mzee Yusuf amesema kuwa muziki
huo kwa sasa umekuwa maarufu kiasi cha kujizolea mashabiki wengi tofauti na
zamani.
Akizungumza na TABIBU jijini Dar es Salaam alisema muziki wa
Taarab wakati unaanza ulizoeleka kama ni muziki wa pwani, lakini kwa sasa ni
muziki unaopendwa na watu wote.
Mzee Yusuph alisema, “pamoja na muziki huo kuwa maarufu,
mimi naendelea kuwa mfalme wa muziki huo nikiwa sina mshindani wa kushika nafasi
yangu. Wamejaribu wameshindwa.”
Mzee Yusuph ambaye pia ni Mkurungezi wa Jahazi Modern
Taarab, alisema anajivunia mafanikio makubwa aliyopata katika muziki huo na
ndiyo maana kwa sasa anafikiria kujenga misikiti kadhaa huku Chanika jijini Dar
es Salaam kama sehemu ya shukrani zake kwa Mungu.
Nyota huyo kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa ‘Mahaba Niue’
chini ya bendi yake ya Jahazi Modern Taarab, bendi aliyoanzisha tangu mwaka
2006.
DK. CHENI 'NIMEKUBALI KUOLEWA'
Na Kennedy Chaya, Dar
Mwigizaji mkongwe nchini Muhsin Awadh maarufu kama Dk. Cheni
amesema, ile filamu yake ya “Nimekubali kKolewa” iloyozuiliwa na Bodi ya Filamu
Tanzania (TFB) kwa kile kilichosemekana kuwa kukiuka maadili ya Kitanzania sasa
iko huru kuingia sokoni.
Akizungumza
na gazeti hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Dk.Cheni alisema bodi hiyo ilimfungia filamu hiyo kwa madai ya kuwepo maudhui
yanayoashiria ushoga, saura ambalo linapigwa vita na Serikali.
“Nilipewa sharti la kufanya
marekebisho katika sehemu zote ambazo bodi hiyo iliona kuwa maadili ya Kitanzania
yalikiukwa, nikasahihisha makosa hayo na sasa filamu hiyo imepitishwa. Hivyo
muda wowote kuanzia sasa itakuwa ikisambazwa katika maeneo mbalimbali nchini,”
alisema Dk.Cheni.
Aidha Dk. Cheni aliongeza kuwa baada filamu yake hiyo kuwa
huru kuingia sokoni atahakikisha anashirikiana vizuri na wadau wanaosambaza filamu
hiyo ili iweze kuwafikia mashabikai wake kote nchini.
Msanii huyo alifafanua kuwa kwa sasa hafikirii kufanya
filamu nyingine mpaka aone matokeo ya filamu yake ya “Nimekubali Kuolewa.”
BEN PAUL: NIMEPATA TABU SANA KWENYE MAPENZI
Na
Juma Diwani, Dar
Nyota
wa muziki wa R&B Bongo, Benard Paul maarufu kama Ben Paul ameliambia TABIBU
wakati wa mahojiano maalum kuwa yupo mapumzikoni mkoa wa Mwanza lakini anajiandaa
kufunga mwaka kwa kufanya kazi kubwa na jamii ili kuonesha upendo.
Msanii
huyo ambaye hivi karibuni alitamba na wimbo wake unaoitwa ‘Upendo’ ambao unaendelea
kufanya vizuri katika redio na runinga mbalimbali nchini alisema kuwa ameamua kwenda
kupumzika Mwanza kutokana na uzuri wa mji huo na kuutaja kuwa ni mji wa pili anaoupenda
baada ya Arusha ingawaje yeye nyumbani ni Dodoma.
Ben
Paul ni msanii ambaye nyimbo zake nyingi zimejikita kwenye mapenzi na nilipomhoji
kwa nini anaimba kuhusu mapenzi sana kuliko kitu kingine alisema kuwa kila anachokiimba
kimeshawahi kumtokea katika safari yake ya mapenzi.
“Kila
nyimbo ninayoimba ya mapenzi inanihusu kwa sababu nimepitia mengi katika mapenzi,”
alisema msanii huyo.
Hata
hivyo, Ben Paul alisema kuwa mpaka hatua aliyofikia kwa sasa kimziki inatokana na
sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki
wake na kusema kuwa hatowaangusha, hivyo
wazidi kumpa sapoti ya kutosha.
No comments:
Post a Comment