Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Thursday, September 25, 2014

Ebola: Liberia yatoa ya moyoni kwa Umoja wa Mataifa



Monrovia, Liberia

Hivi karibuni viongozi wa Liberia wameamua kujitokeza mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuihakikishia taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa wameshindwa kuidhibiti homa ya Ebola, wakati ambapo Umoja huo umekuwa ukiahidi kuongeza juhudi za kimataifa ili kuzuia virusi hivyo.

Waziri wa Ulinzi wa Liberia, Brownie Samoukai, alitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuingilia kati, ili kuzuia ugonjwa huo wa Ebola, huku akisisitiza kuwa Ebola imekua ni tishio kwa usalama wa taifa hilo.

“Usalama wa Liberia uko hatarini kutokana na ugonjwa wa Ebola, ambao umekua ukisababisha vifo vya watu, na kuendelea kuenea katika maeneo mbalimbali ya nchi, ukiwemo mji mkuu wa Liberia, Monrovia”, alisema waziri Brownie Samoukai.

Mbali na hayo, Umoja wa Afrika AU umesema kuwa unatuma timu kadhaa za wataalam wa kutiba magharibi mwa Afrika kwa minajili ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa nchi ambazo zimeathirika zaidi na mlipuko wa homa ya Ebola zinahitaji zaidi uangalizi wa kitiba ili kuweza kukabiliana na janga hilo.

Umoja wa Afrika unataraji kutuma watu 100 ambao miongoni mwao watakuwemo madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine wa huduma za kitiba ili kuunga mkono jitihada zinazotekelezwa sasa ili kuzuia kuenea kwa homa ya Ebola.

Homa hiyo ya Ebola inaonekana kuwa na nguvu zaidi tangu ilipogundulika mwaka 1976, na imekua vigumu kuidhibiti. Homa hiyo imesababisha vifo vya watu 2296 huku watu 4293 wakiwa wameambukizwa virusi vya Ebola. Nchini Liberia pekee watu 1224 wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa Ebola, Shirika la Afya Duniani WHO, limethibitisha.

Pamoja na nchi hizo kuonekana kuathirika zaidi, lakini pia vifo vya watu saba vimeorodheshwa kutokea nchini Nigeria ikiwa ni taifa linalostawi kiuchumi barani Afrika

Sambamba na hayo, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, ambako kunaripotiwa aina nyingine ya Homa ya Ebola tofauti na ile inayoshuhudiwa Afrika ya magharibi. imeordhesha vifo vya watu 32 ambao wamefariki kutokana na Homa hiyo.



No comments:

Post a Comment