Na Firdaws Alinus
Karibu tena mpenzi msomaji wa TABIBU, leo tunalo mapishi ya mkate wa mbogamboga. Chakula hiki tumezoea
kukikuta hasa hotelini au kwenye sherehe na kwenye ndege, watu walio wengi
huamini kwamba kuandaa chakula hiki nyumbani ni gharama sana. Chakula hiki kina
faida kiafya katika mwili wa mwanadamu.
Mahitaji
Mafuta ya mmea vijiko vitano
Vitunguu maji na swaum.
Pilipili mboga (hoho)
Karoti, zukini,
Kijiko kimoja cha chumvi.
Nyanya,
Hamira chenga, unga wa ngano,
Mayai 2
Sukari na maji au maziwa kikombe 1.
Jinsi ya kuandaa
Tengeneza donge la mkate kwa
kuchekecha unga wa ngano pamoja na hamira, weka sukari, chumvi na mayai kisha ongeza
maji na uanze kuchanganya changanya kwa kukanda kama chapati tengeneza madonge madogomadogo
ns usukume donge moja kama chapati kwenye ubao na ikishakamilika kuwa kama
chapati tandaza kwenye kontena ya silva yenye pembe 4 na uache kidogo kwa dakika
35 hadi 45.
Wakati unasubiri hizo dakika hizo
kufika kaanga vitunguu maji na swaumu na uendelee kukaanga mpaka rangi ibadilike
kuwa ya kahawia kisha weka pilipili nyanya, hoho, karoti, zukini, pasley pika
kwa dakika 20 hadi 30 ikiwa tayari jaza rosti hiyo katika donge lililo tandazwa
katika kontena ya silva kisha chukua donge lingine lililosukumwa kama chapatti
na utandaze juu ya rosti iliyopo kwenye donge ifunge vizuri kwa madonge hayo ya
ngano.
Baada ya hatua hizo zote unaweza
ukaoka kwa kutumia jiko la mkaa au oven ya umeme.
Faida za mkate wa mbogamboga.
Waisrael ni watumiaji wakubwa wa mkate
wa aina hii na ni chakula ambacho hubadilisha sukari pia husaidia kufyonzwa kwa
mafuta mwilini kwa sababu ya ‘chlorine’ na
kuna kiasi kidogo ‘calcium’ pia huboresha neva na kuimarisha mifupa na
meno pia tatizo la kutopata usingizi hudhibitiwa ukuaji wa mwili hujengwa na
selenium na zink husaidia uyeyusho na kufyonza vitamin C.
Mpenzi msomaji hadi kufikia hapo
tutakuwa tumehitimisha mapishi yetu ya leo, ni matumaini yangu kuwa umefurahia
mapishi. Tukutane tena wiki ijayo kwa muendelezo wa mapishi.
No comments:
Post a Comment