Dk. Geoffrey C. Lusanzu
Mpenzi msomaji wa blog ya TABIBU, hii ni makala ya kwanza katika mfululizo wa elimu ya afya juu ya kujikinga na kujitibu maradhi ya baridi yabisi (arthritis). Baridi yabisi ni mkusanyiko wa maradhi yanayotesa watu wengi katika siku za hivi karibuni za maisha ya kisasa. Maradhi haya ni makali kiasi kwamba humtesa mtu na kumfanya kuwa mlemavu na hata kupelekea kifo wakati mwingine.
Nini husababisha maradhi haya?
Ni uwepo wa sumu nyingi za tindikali mbaya katika mwili (uric acid) na wakati mwingine ni maambukizo ya bakteria, virusi, na matatizo ya kinasaba.
Uric acid ni sumu gani?
Ni tindikali mbaya inayotengenezwa mwilini kutokana na maozea (putrid mass) ya vyakula vya nyama, mafuta ya wanyama, seli hai za mwili zilizokufa mwilini pamoja na vyakula na vinywaji vingine vingi visivyo vya asili (vyakula mtumba na vya anasa).
Inatokeaje viungo kuuma na kuvimba?Kadri ‘uric acid’ zinapotawala mwili ndivyo damu hudhoofishwa nguvu yake ya kiutendaji na misuli hushambuliwa na vipenyo vyake huziba. Hivyo ‘uric acid’ huwasha na kukereketa katika minofu sehemu ambako damu haifiki kwa kiwango kinachotakiwa. Hali ya kuvimba huwa ni matokeo ya juhudi za mwili kujihami na kujinusuru na ‘uric acid.’
Uric Acid huvamia viungo gani?
Kadri tindikali mbaya (uric acid) inavyotapakaa mwilini ndivyo mwili hujitahidi kuiondoa kwenye mkondo wa damu na hivyo kuitupa kwenye minofu au kwenye ngozi, hapo ndipo figo, ini, moyo, tezi dume, kongosho na ubongo ambapo misuli midogo ya damu katika viungo hivyo hushambuliwa na kuziba, ndipo viungo hivyo na vingine vingi hudhoofika na kuteteleka kiutendaji huku vikileta dalili za kuugua.
Orodha ya vyakula vinavyotengeneza ‘uric acid’?Orodha hii ndiyo huchangia kutengeneza ‘uric acid’ nyama za aina zote, mafuta ya wanyama , mafuta yenye lehemu (cholesterol) yaliyotengenezwa kiwandani, tumbaku, pombe za aina zote, bangi na mihadarati, kahawa, vidonge vya kemikali, vyakula vya rojorojo vya kianasa, maziwa, soda, kola na mikate mitamu iliyotengenezwa kwa hamira za kiwandani.
Naweza kutibiwa na kupona maradhi ya baridi yabisi?Kuwahi ugonjwa ni kupona, lakini kukawia kutibiwa ni kujileteleza ulemavu na pengine kifo kabisa. Hivyo ni vizuri ukawahi kupata matibabu mapema mara unapohisi dalili za ugonjwa huu.
Naweza kutibiwa na kupona maradhi ya baridi yabisi?Kuwahi ugonjwa ni kupona, lakini kukawia kutibiwa ni kujileteleza ulemavu na pengine kifo kabisa. Hivyo ni vizuri ukawahi kupata matibabu mapema mara unapohisi dalili za ugonjwa huu.
Dawa gani zinatibu maradhi ya baridi yabisi?Dawa za kizungu (vidonge) na dawa za mitishamba (za asili) zote zinatibu kikamilifu endapo tu hazitachanganywa na kemikali mbaya, kwani kemikali mbaya inapoingia mwilini hugeuka kuwa tindikali nyingine mbaya mno ambayo huunga mkono ‘uric acid’ na vyote kwa pamoja kuuangamiza mwili taratibu pasipo utetezi.
Mgonjwa wa maradhi haya ale chakula kipi ?
Maji ni muhimu sana, hivyo mgonjwa anywe kila siku lita 2 hadi 4 za maji safi na salama. Pia ajikite kula vyakula vya asili zaidi ambavyo ni pamoja na mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali hasa yale yasiyo na sukari (citrus,) maharage ya soya pamoja nakufanya mazoezi ya viungo ya kutosha.
Ikiwa umeathirika tayari ni vizuri ukaenda hospitali au wasiliana nami kwa kupata tiba njema na kwa muda mfupi au kwa kupata nasaha.Usikose muendelezo wa makala haya sehemu ya pili!
Makala haya yameletwa kwenu na Geoffrey C. Lusanzu, ambaye ni daktari na Mkurugenzi wa kliniki ya Tiba Mbadala TANAMEREC, Kibanga, Kasulu, Kigoma. Au wasiliana nao kupitia Email: selemtiba@gmail.com. Au simu namba 0759 022 054 / 0714 284 804.
ITAENDELEA…
No comments:
Post a Comment