Ni ile hali ya
mwanaume kuwahi kutoa manii wakati anashiriki tendo la ndoa, kuwahi mapema na
haraka zaidi pasipo maamuzi yake au bila kukusudia.
Kwa kawaida
mwanaume anatakiwa kutoa manii au kufika kileleni dakika 5 hadi
15 na endapo atafika kileleni kabla ya dakika 5 ndo tunaita ana (premature ejaculation)
Tafiti
zinaonesha wanaume wengi sana wana hili tatizo na inakadiriwa kuwa kati ya
wanaume 3 mmoja huwa na tatizo hili..
Sababu zinalopelekea kuwahi kufika
Kileleni
- Magonjwa yanayoathiri tezi dume (Pro static Disorder.) Tezi dume ni kiungo kimojawapo kati ya viungo vya uzazi wa mwanaume ambayo kazi yake kubwa ni kutoa manii (semen). Bacteria wanaweza kushambulia na kusababisha ikapoteza ufanisi wa kazi yake au kupungua kwa homoni zinazoisaidia uzalishaji wa manii, kuathirika kwa hii tezi dume kunapelekea zaidi tatizo hili la kuwahi kufika kileleni (Premature ejaculation)
- Kujichua (masturbation), kunapelekea misuli ya uumekuwa dhaifu na akiwa dhaifu mwanaume anakua hana uwezo wa kujizuia anapokaribia kufika kileleni na kutokana na kunapelekea mishipa inayopeleka damu kwenye uume kusinyaa hivyo kupelekea damu kutofika ya kutosha kwenye uume na kufanya uume usimame legelege. Ambapo pia huweza kuwa chanzo cha tatizo hili. 3.Uharibifu wa mishipa inayotokana na utoaji wa manii, hususani mtu anapokuwa amepata ajali au kufanyiwaupasuaji(operation)
- Msongo wa mawazo (stress), pia huweza kuathiri utendaji wa ‘hypothalamus,’ ambayo inahusika katika utoaji wa homoni ambazo zinaimarisha viungo vya uzazi. Stress inaathiri utendaji wa ‘hypothalamus,’ ambayo inahusika katika utoaji wa homoni ambazo zinaimarisha viungo vya uzazi vya mwanaume hasa uume.
- Kuwa na wasiwasi, uoga, kutojiamini wakati wa tendo la ndoa.
- Migogoro, matatizo ya kimahusiano. Mfano: ugomvi.
- Kushindwa kufanya maandalizi mazuri kabla ya tendo
- Tabia ya kurithi
- Kuruhusu hali yoyote isiyo ya amani na utulivu itawale katika fikra zako.
- Ulevi au kunywa pombe kupita kiasi
- Uvutaji wa sigara, ambao hupelekea kusinyaa kwa mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume.
Matibabu
Matibabu ya
tatizo hili hutegemeana namna mtu atakavyokuwa ameathirika na hutegemeana na
chanzo cha kuathirika kwa kiungo hicho. Hata hivyo, kuna kanuni maalum ambazo
lazima zizingatiwe katika kurudisha hali hiyo kuwa vizuri, lakini pia kuiepuka
kabisa.
Unashauriwa
kufika kwa wataalam wa afya endapo unasumbuliwa na tatizo hili ili kuweza
kubaini ni nini chanzo cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi zaidi.
Makala nyingine
nzuri na za kuelimisha kuhusu afya yako hakikisha hupitwi na gazeti la TABIBU
kila Alhamis kwa shs. 500/= tu.
No comments:
Post a Comment