Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Wednesday, September 24, 2014

Tatizo la kuvimba kwa korodani




Ni ugonjwa unaoathiri korodani na kuifanya ivimbe, ugonjwa huu unaweza kusababishwa na bacteria au virusi.

Kutokana na maambukizi ya vimelea hivi bacteria na virusi huweza kupelekea kuathirika kwa korodani moja au zote mbili kwa wakati mmoja.

Lakini kabla ya kwenda mbali zaidi ni vizuri kukumbuka kwamba korodani kazi yake kubwa ni kuzalisha mbegu za kiume.

Chanzo cha tatizo hili
· Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni aina ya virusi vijulikanvyo kama ‘mups virus,’ kwa hiyo virusi hawa endapo watashambulia korodani husababisha korodani kuvimba na kupunguza utendaji kazi wake.

· Maambukizi yanayotokana na vimelea (bacteria) inawezekana ni vimelea wanaosababisha tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) na magonjwa mengine ya zinaa kama Kaswende, Kisonono.

· Kuumia kwa korodani, pengine inaweza kuwa chanzo ni ajali au michezo ya hatari, hali kama hiyo pia huweza kuchangia korodani kuvimba.

· Maambukizi ya ‘epididymis’ ni chanzo kingine cha tatizo hili, ambapo ‘epididymis’ ni mrija ambao kazi yake ni kutunza mbegu za kiume baada ya kuzalishwa kutoka kwenye korodani.
Watu walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu.
· Kama mtu hakupata chanjo ya kuzuia virusi aina ya ‘mumps’ basi mtu huyo atakuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.

· Kupata tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) mara kwa mara.

· Watu ambao hufanya mapenzi na watu tofauti tofauti mara kwa mara nao huwa katika hatari ya kupata tatizo hili.

· Kufanya mapenzi na mtu mwenye magonjwa ya zinaa

· Kama mtu alishawahi kupata magonjwa ya zinaa pia yuko kwenye hatari ya kupata tatizo hili.

Dalili za kuathirika kwa ugonjwa huu

Dalili za tatizo hilo ni pamoja na kuvimba kwa korodani moja au zote mbili, maumivu makali ya korodani, homa kali, kichefuchefu na hata kutapika na maumivu sehemu za mitoki.

Matibabu ya tatizo hili

Matibabu ya ugonjwa huu hutegema sana na chanzo cha maambukizi kati ya bacteria au virusi kwa hiyo baada ya uchunguzi kubaini nini chanzo matibabu ndipo hufuatia na yanaweza kuanzia kwa kuua vimelea vilivyosababisha tatizo hilo kwa kutumia kutumia dawa.

Athari ambazo hujitokeza endapo mgonjwa atachelewa kupata matibabu
· Kunywea kwa korodani moja au zote mbili.

· Kuwa na jipu au vijipu kwenye korodani ambalo limeathirika na maambukizi ya bacteria.

· Utasa, hii ni kutokana na kuzalishwa ‘testosterone hormone’ kwa kiwango kidogo ambayo inasaidia uzalishaji wa mbegu za kiume

· Upungufu wa nguvu za kiume.

Namna ya kuepuka ugonjwa huu.
· Wapenzi wawe na utaratibu wa kupima afya zao hususani magonjwa ya zinaa hasa kabla ya kushiriki tendo la ndoa.

· Kuzingatia matumizi ya kondomu wakati wa tendo la ndoa hususani kwa wale ambao hawajapima afya zao.

· Kupata matibabu ya uhakika pale unapogundulika una tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) au magonjwa ya zinaa.

· Endapo utakuwa na miongoni mwa dalili hapo juu ni vizuri ukawahi hospitali kupata matibabu mapema.



Makala hii imeletwa kwenu na kituo cha Victoria Therapies kilichopo Mtoni Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Au unaweza kuwasiliana nao kupitia simu namba 0658 027 027.

Endelea kufuatilia makala hizi za afya ya uzazi kwa wanaume kupitia gazeti lako la TABIBU linalopatikana mtaani kila siku ya Alhamis kwa shilingi 500/= tu

2 comments: