Dk. Febronia Kalongoti
Habari mpenzi msomaji wa
blog yetu ya TABIBU, natumaini mzima wa afya. Bado tunaendelea kupeana mambo
mengi mazuri ambayo pengine huyajui au unayajua kwa uchache.
Leo tunakuletea tunda la
komamanga na faida zake mwilini.
Komamanga ni tunda lenye
asili ya India na Persia kwa jina la kisayansi ni Punica Granatum, lakini
lililetwa Marekani na wawekezaji wa Kihispania na kwa sasa limejulikana dunia
nzima.
Tunda hili hustawi sana kipindi
cha mwezi wa tisa na wapili, na huweza kushamiri sana katika hali ya hewa ya
joto, lakini pia komamanga ni hodari katika kumudu hali ya ukame.
Kama hujawahi kula
komamanga huwezi jua nini unakosa, lakini ukweli ni kwamba komamanga sio tunda
tu bali ni chakula kilichojawa na afya ya vitamin, madini pamoja na virutubisho
vingine vingi vinavyoweza kufanya miili yetu kuwa na afya na nguvu tele.
Tunda hili pia
linajulikana kama ‘Granada’ au Tufaa
la kichina (Chinese Apple), hali kadhalika tunda hili hufahamika zaidi kwa
uzuri wa juisi yake,
Mkomamanga huweza kukua
kwa urefu wa mita 5 hadi 8 na ina uzito wa gram 200, huku ikiwa na ‘calories’ za kutosha. Ambapo katika
gram 100 komamanga huweza kutupatia kiasi cha 83 ‘calories,’ pia tunda
hilo linaelezwa kutokuwa na ‘cholesterol’
wala mafuta.
Virutubisho vinavyopatika katika komamanga
Ina vitamin C kwa wingi
Vitamin B5
Vitamin A
Vitamin E
Madini kama Potassium na Iron
Mbegu zake ni chanzo
kizuri cha nyuzi nyuzi ‘fiber’
Unywaji wa juisi ya
mbegu za komamanga utakupa dozi kamili ya kansa, pia husaidia mtiririko wa damu
kwenda vizuri katika mishipa ya damu, ambayo husaidia presha ya damu na
kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kiharusi.
Hulinda meno kuzuia
kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu bakteria na maambukizi ya virusi ndani ya mwili,
lakini pia husaidia kutibu madhaifu ya tumbo kama kuharisha, kutopata choo na
maambukizi mbalimbali, matatizo sugu ya gesi tumboni hasa vidonda vya tumbo,
hupunguza tindikali tumboni n.k
Matumizi
Hutumika kama tunda
likiwa bichi
Hutumika kama juisi
Hutumika likiwa
limepikwa.
Natumaini mpenzi msomaji
utakuwa umepata kujua umuhimu wa tunda hili kiafya mwilini.
Kumbuka Miracle Food hutoa mafunzo ya kutengeneza
maziwa ya soya, almond, mahindi machanga, karanga na dengu. Pia hutoa matibabu
ya matatizo mbalimbali yanayosumbua mwili.
Kwa mawasiliano na huduma nyingine za kiafya na
ushauri fika Kariakoo mtaa wa Msimbazi jengo la Klubu ya Simba ghorofa ya tatu
au piga simu namba 0755 -093 418 na 0715 – 093 418, Facebook: febronia miracle food au Google:
miracle food clinic & counseling au Email: miraclefoodfebronia@yahoo.com
Kwa makala nyingine nyingi kama hizi hakikisha,
hupitwi na nakala yako ya gazeti la TABIBU kila
siku ya Alhamisi kwa shilingi 500/= tu.
No comments:
Post a Comment