Wataalam wa afya wakivuta pumzi baada ya kutoa huduma kwa wagonjwa. |
Waziri wa Ulinzi wa Liberia ameonya
kuwa Ebola inatishia kuwepo kwa taifa hilo wakati virusi hivyo hatari
vikisambaa mithiri ya “moto wa kichakani”. Huku Shirika la Afya Duniani (WHO)
likiarifu kuongezeka kwa idadi ya vifo.
Hata hivyo, taarifa hizi zinafuatiwa
na baada ya kutabiriwa kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yatafikia kiwango cha juu
kote Afrika Magharibi, Aidha WHO imeeleza kuwa Liberia ambayo imeshuhudia nusu
ya jumla ya idadi ya vifo vilivyoripotiwa na huenda ikatarajia kupunguza tu kwa
usambaaji wa virusi hivyo, na wala siyo
kuzuia.
Naye Waziri wa Ulinzi wa Liberia
Brownie Samukai aliuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa
ugonjwa wa ebola unasambaa kwa kasi kama moto wa kichakani, huku ukikiteketeza
kila kitu njiani mwake.
WHO imesema idadi ya vifo vya ebola
imeongezeka hadi kufikia 2,296 kati ya visa vya maambukizi 4,293 nchini
Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria kufikia Septemba 6. Takribani nusu ya
maambukizi yote yalitokea katika kipindi cha siku 21 zilizopita.
Aidha, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa
Mataifa nchini Liberia, Karen Landgren naye alisema kuwa ugonjwa huo unasambaa
nchini humo ''Bila huruma''.
Takwimu za hivi karibuni za WHO zinaonesha
kuwapo kwa usambaaji wa kiholela wa ugonjwa huo na hali ikionesha kuwa ugonjwa
huo hujipenyeza katika jamii zilizojaa watu bila vifaa maalum vya matibabu na
zinazokosa kampeni za uhamasisho wa umma kuhusiana na mlipuko huo.
Wakati hayo yakiendelea Mkuu wa
Kitengo cha Magonjwa wa WHO Sylvie Briand alisema lengo la sasa nchini Senegal
na Nigeria ni kuhakikisha wanazuia kabisa maambukizi ya ugonjwa huo. NA. DW.
No comments:
Post a Comment