Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Thursday, October 2, 2014

Kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa kwa mwanaume



Na Dk. Emmanuel James

Tatizo la mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa (hypoactive sexual desire disorder for men ) ni ile hali ya mwanaume kukosa msisimko na hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Takwimu zinaonesha kwamba kila wanaume watano mmoja anakabiliwa na tatizo hili, huku tatizo hili likionekana kuwa ni chanzo kikubwa cha kujishusha thamani kwa baadhi ya wanaume na kukosa kujiamini.

Lakini pia tatizo hili limeonekana kuchangia msongo wa mawazo kwa wanaume wengi wanaosumbuliwa na tatizo hili.

Kukosa hamu ya kufanya mapenzi kunapelekea wanaume wenye tatizo hili kupunguza hata ukaribu na wenzi wao kwa kuogopa pengine mpenzi wake atagundua kuwa anatatizo hilo, hivyo wanaume wengi wenye tatizo hili hutumia sababu mbalimbali za uongo kwa wapenzi wao kwa lengo la kupunguza ukaribu nao.

Chanzo cha tatizo hili
  • Umri, kwa mwanaume anavyozidi kuongezeka kiumri hivyo hivyo pia hupunguza shahuku na hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
  • Msongo wa mawazo (stress), kuwa na msongo wa mawazo unaotokana na migogoro ya kifamilia, mahusiano , hali ngumu ya kiuchumi au magonjwa yananyoathiri mfumo wa fahamu (mental disorder) yanaweza kuwa chanzo cha tatizo hili.
  • Matatizo ya kiafya (deseases), baadhi ya magonjwa huweza kumsababishia mwanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa. Mfano wa magonjwa hayo ni pamoja na presha ya kupanda, mafuta menge mwilini, kisukari, UKIMWI n.k
  • Upungufu wa vichocheo vya hisia na hamu, (Hormonial Inbalance), kutolewa kwa kiwango kidogo cha kichocheo kijulikanacho kitaalam kama ‘testosterone’ ambacho huhusika na kuamsha hisia, msisimko na hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanaume, hivyo pale kichocheo hicho kinapopungua kinaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha tatizo hili na mara nyingine huweza kupelekea matatizo mengine kama asthma, kisukari n.k
  • Utumiaji wa baadhi ya madawa pia huweza kuwa chanzo cha tatizo hilo, hususani madawa yanayotumika kwa wagonjwa wa presha ya kupanda, kisukari, matatizo ya akili n.k. 
  • Upungufu wa “Dopamine” ambayo hutolewa na ubongo na kazi yake kubwa ni kumfanya mtu ajisikie vizuri pamoja na kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa. 
  • Uchovu pia ni miongoni mwa sababu za tatizo hili.
  • Unene kupita kiasi, kwa maana kwamba kadri unene unavyoongezeka huathiri uzalizaji wa ‘testosterone hormone,’ ambayo husaidia kuleta hamu ya kushiriki mapenzi.
  • Ulevi wa pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeini, heroin nazo pia ni sababu za tatizo hili.


Matibabu 
Matibabu hutegemea na chanzo cha tatizo, lakini kwa ujumla utumiaji wa baadhi ya vyakula huweza kukusaidia kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na ndizi, parachichi, tikitimaji, zabibu, tangawizi, pilipili,pweza na ngisi hivyo ni baadhi ya vyakula vinavyoweza kusaidia kuondokana na tatizo hili.

Mwanaume mwenye tatizo hili huweza kukabiliwa na yafuatayo endapo hata pata matibabu ya maepema.

Msongo wa mawazo ambao utapelekea kusababisha matatizo mengine kama, presha ya kupanda, vidonda vya tumbo, n.k

Kushindwa kusimamisha uume.

Kushindwa kabisa kumridhisha mwenza wako na hatimaye kuvunja ndoa au uhusiano. 

Ushauri
Ni vizuri kuwahi mapema kuwaona wataalam mara tu unapohisi kuwa na tatizo hili, itakusaidia kupata utatuzi wa kina juu ya hili.

Kwa ushauri, vipimo pamoja na matibabu unaweza kutembelea kituoni kwetu Victoria Therapies kilichopo Mtoni Kijichi Manispaa ya Temeke. Au wasiliana nasi kupitia namba ya simu ifuatayo; 0658 027 027.

No comments:

Post a Comment