Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Saturday, October 11, 2014

Kituo cha Ebola Tanzania kukamilika ndani ya wiki mbili

Madktari maalum wa ugonjwa wa Ebola katika kituo cha Ebola - Hospitali ya Temeke.

Na Juma Diwani, Dar

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea kituo maalum cha kupokea wagonjwa watakaobainika kuwa na ugonjwa wa Ebola katika Hospitali yaTemeke, jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Dk. Jakaya alibaini mapungufu mbalimbali ikiwemo uzio na mfumo mbovu wa maji taka na kuagiza marekebisho yafanyike haraka ili kuweza kukabiliana na Ebola wakati wowote itakapoingia nchini.

Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa Afya Mkoa wa Dar es Salaam, Sister Mathew alisema kuwa ukarabati unaendelea kwa haraka ilikuwa tayari wakati wote. “Ukarabati wa kituo unaendelea tena kwa haraka kama alivyoagiza Rais ili kuwa tayari na kukabiliana na ebola wakati wowote itakapoingia nchini ingawaje hatuombei hilo litokee” alisema Sister Mathew.

Sister aliongeza kwa kusema kuwa ukarabati huu unafanywa na mafundi kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) na kwa muda wa wiki mbili ukarabati huo utakuwa umekamilika.

“SUMA JKT ndio wanafanya ukarabati na kwa muda wa wiki mbili watakuwa wameshamaliza na inawezekana wakamaliza mapema zaidi kutokana na kasi waliyokuwa nayo katika ujenzi.”


Hata hivyo, aliwataka wananchi kuwa waangalifu endapo ebola itaingia nchini kwani ni ugonjwa hatari kwa sasa.

No comments:

Post a Comment