Dk. Fadhili Emilly
Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu asili yake ni nchini India na Burma. Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame.
Hapa nchini Tanzania, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini pia.
Jina hili la ‘mwarobaini’ linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini, huku majani yake na mbegu zikitumiwa kama tiba kwa miaka mingi katika nchi mbalimbali duniani.
Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni pamoja na matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, saratani, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k.
Pia matawi ya mti huu hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.
Hali kadhalika mafuta ya mbegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni, lakini pia mbegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani.
Baada ya kufahamu baadhi ya faida mbalimbali za mti wa mwarobaini, leo nitakufundisha namna ya kutumia mti wa mwarobaini kujitibu magonjwa ya ngozi.
Mahitaji
Majani ya mti wa mwarobaini.
Sufuria
Mwiko
Jiko la gesi, mkaa au jiko la mafuta.
Hatua za kufuata
1. Chukua majani mabichi ya mti wa mwarobaini na uyaweke kwenye sufuria.
2. Chukua sufuria yako yenye majani ya mti wa mwarobaini na uiinjike kwenye jiko lenye moto wa wastani.
3. Chukua mwiko wako na uanze kuyakoroga majani yako taratibu hadi yakauke bila kuungua.
4. Majani yako yakishakauka, ipua sufuria yako, chukua majani yako yaliyokauka, yasage kisha hifadhi unga unga wako kwenye chombo cha plastiki.
Matumizi
Tumia vijiko viwili vya chai kwenye kikombe cha robo lita chenye maji ya moto, fanya hivyo mara mbili kwa siku kwa muda wa siku ishirini na moja.
Makala haya yameletwa kwenu na The Fadhaget Sanitarium Clinic, ambao hutoa huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali kwa kutumia mimea asilia. Makao makuu yao ni Mbezi Beach Afrikana njia ya Salasala, Dar es Salaam. Au unaweza kuwasiliana nao kupitia namba; 0712 705 158, 0757 931 376, 0787 705 158, 0774 505 158. Pia unaweza kuwapata kupitia www.tv51.co.tz
No comments:
Post a Comment