Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Thursday, August 28, 2014

Kokwa la embe huweza kuondoa maumivu wakati wa tendo la ndoa


Dk Mandai
Maumivu wakati wa tendo la ndoa huwakabili baadhi ya watu na kusababisha walichukie au kukosa hamu ya kufanya tendo hilo.

Mara nyingi maumivu yanayotokea mwanzoni wakati wa tendo la ndoa halafu yanapotea baadaye, hali hii husababishwa na upungufu wa ute unaoilainisha njia ya uzazi na mara nyingi hutokana na maandalizi hafifu wakati wa tendo husika.

Wakati mwingine hali hii hutokea baada ya mwanamke kumeza dawa zinazohusisha majimaji ukeni kama vile dawa za kuzuia uzio na nyinginezo.

Adha, tatizo la maumivu wakati wa tendo la ndoa huweza kusababishwa na athari za kisaikolojia anazokuwa nazo mwanamke. Mfano kama mwanamke aliwahi kubakwa au kufanyiwa vitendo viovu mara nyingi mwanamke wa aina hii huweza kuwa na hali ya kutohisi hamu ya tendo la ndoa.

Wanawake wenye uwezekano wa kukumbwa na tatizo hili.
·      Niwale ambao muda wao wa kupata hedhi umekoma, hii ni kwa sababu baadhi ya vichocheo (homoni) vinavyochochea kutolewa kwa majimaji ili kulainisha njia ya uzazi hupungua kwenye damu, na wengine ni wale wenye matatizo ya maambukizi ya magonjwa katika viungo vyao vya uzazi hususani magonjwa ya zinaa.

·      Maambukizi kwenye njia ya mkojo hasa kwenye kibofu cha mkojo huleta maumivu wakati wa tendo la ndoa.



·      Wanawake wenye matatizo sugu ya kukosa choo wao wanauwezekano mkubwa wa kupata maumivu haya.

·      Endapo mwanamke atafanya tendo la ndoa kipindi kifupi mara baada ya kujifungua huweza kupata maumivu wakati wa tendo hilo. Mwanamke anapo jifungua viungo vyake vya uzazi huchukua muda mrefu hadi kurudi katika hali yake ya kawaida, hivyo basi anaposhiriki tendo la ndoa muda mfupi baada ya kujifungua atajisikia maumivu. Pia tatizo hili huwapata wanawake waliojifungua kwa kuongezwa njia ya uzazi.

 Maumivu kwa wanaume
Wanaume huweza kupatwa maumivu ya aina hii wakati wa tendo lenyewe au wakati wa kutoa mbegu. Pia maumivu haya husababishwa na maambukizi au vidonda kwenye ‘gland,’ ambayo huruhusu mbegu kutoka ‘prostate grand.’

Maumivu kwa wanaume pia husababishwa na maambukizi kwenye ngozi inayofunika uume na magonjwa ya malengelenge na baadhi ya magonjwa ya zinaa mara nyingi maambukizi haya husababishwa hata wakati wa kusimama. Hizo ni baadhi ya sababu, ambazo mara kwa mara husababisha tatizo hili.

Athari
Ni jambo la muhimu kwenda hospitali unapokuwa na tatizo hili kuliko kukaa kimya, jitahidi kumuelezea namna maumivu hayo yanavyokutokea. Mfano utapaswa kumueleleza daktari maumivu unayoyapata yana muda gani na hutokea baada ya tendo lenyewe au ni tofauti. Hivyo daktari atafahamu ni dawa gani akupatie.

Magonjwa ya zinaa yanachangia tatizo hili, hivyo ni vyema kwenda na mwenza wako mkachunguzwe na kutibiwa wote. 

Tiba hufanyika kwa kutegemea sababu iliyosababishwa na kumuona mtaalamu wa matatizo ya kisaikolojia kwa msaada zaidi, wale wenye tatizo la kisaikolojia wanashauriwa kumuona daktari wa matatizo ya kisaikolojia kwa msaada zaidi.

Kinga
·      Ni muhimu kuzingatia usafi kwani hupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya maambukizo.

·      Kila mtu anatakiwa kumuandaa mwenzake wakati wa tendo hili ili kusaidia majimaji ya kulainisha njia ya uzazi yatoke ya kutosha
·      Wale wenye njia kavu zaidi mafuta maalumu ya kulainisha hutumika, isipokuwa hakikisha hautumie Vaseline au mafuta mengine ya mgando kwani yanaweza kurahisisha kupata maambukizo ya magonjwa.

·      Kwa wanawake hakikisha haushiriki tendo la ndoa mara baada ya kujifungua subiri angalau baada ya wiki sita.

Tiba
Chukua kokwa la embe ponda ponda kausha au twanga, kisha utapata unga wake ambao utatumia katika uji mwepesi 1x3 kwa muda wa siku 14.


Makala nyingi kama hizi unaweza kukutana nazo kupitia gazeti la TABIBU kila siku ya Alhamis kwa shilingi 500/=  tu.

No comments:

Post a Comment