Dk Edger Kapagi
Kitunguu ni mojawapo ya mimea ambayo wanadamu wamekuwa wakikuza kwa
muda mrefu sana. Asili yake ni Persia. Kitunguu kimelimwa katika bonde la Mto Nile
miaka 6000 kabla ya kristo.
Kwa sasa kinalimwa Ulaya, Misri, America, India, China, Japan, Malaysia
na Africa mashariki na kati nk.
Katika nchi nyingi kitunguu hakiwezi kukosekana jikoni. Bila shaka,
kinatumiwa kwa njia mbalimbali kama vile vyakula tofauti, na dawa. Pia kinaweza
kufanya utokwe machozi. Hali kadhalika kitunguu ni mojawapo ya mimea
inayochanua maua maridadi.
Hata hivyo, watu wengi ulimwenguni hutumia kitunguu kilicho na
shina lenye tabaka za mviringo ambalo hukua chini ya ardhi. Aidha, vitunguu
huwa na rangi tofauti, tofauti kama vile nyeupe, manjano, kahawia, kijani,
nyekundu na zambarau.
Unaweza kula vitunguu vikiwa vibichi au vikiwa vimepikwa. Pia
unaweza kula achali ya vitunguu, vitunguu vilivyokaushwa, vilivyosagwa na
vilivyokatwakatwa.
Ni wazi kuwa kitunguu ni mmea wa ajabu, hata kama kitafanya utokwe
na machozi. vitunguu huboresha sana afya ya watu, kwani huwa na protini,
mafuta, nyuzinyuzi, madini, wanga, kalisiumu, fosforasi, chuma, carotene, ‘thiamine B1 niacin B3, riboflavin B2,
sulphur, asidi askobiki au vitamin C na K.
Hata hivyo, kwa miaka mingi vitunguu vimetumiwa hasa kwa matibabu.
Hata leo vinatumika kutibu magonjwa mbalimbali kama vile mafua, kuvimba koo,
utando mgumu wa mafuta katika mishipa ya damu, ugonjwa wa moyo, kisukari, pumu,
kuzuia lehemu (cholesterol), uvimbe, kuganda kwa damu ndani ya mishipa, tambazi,
kusinyaa kwa ini (cirrhosis), vidonda, kuharisha, kupunguza ‘uric acid’, ‘hemorrhoids,’ kikohozi, ‘bronchitis,
’freckles,’ kipindupindu, kuuma sikio, kukuza nywele, hufaa kwa wenye
matatizo ya nguvu za uzazi. (hapa hakikisha unatibu kilichosababisha kupungua
kwa nguvu za uzazi).
Magonjwa mengine ni matatizo ya meno, matatizo ya ini, matatizo ya
ngozi, maumivu ya viungo na ‘arthritis’
ikichanganywa na mafuta ya haradali, maumivu ya kichwa, majipu, matatizo ya
tumbo na pia vitunguu hutumiwa katika dawa za kusafisha vidonda na mengineyo
mengi. Kitunguu kinapendwa sana tutumie kwa ajili ya afya zetu.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi
mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi
inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi
(Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa
gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni
pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi
wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo
ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu
kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi
na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua
Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
Kwa makala nyingi na nzuri kama hizi hakikisha hupitwi na gazeti la TABIBU kila siku ya Alhamisi kwa shilingi 500/= tu.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
No comments:
Post a Comment