Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Wednesday, August 27, 2014

Matatizo ya mkojo mchafu UTI




Dk Mandai
Mkojo mchafu (UTI) ni matatizo katika njia ya mkojo ambayo huchangiwa na maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Matatizo ya UTI husababishwa na vimelea (bacteria) ambavyo huingia katika njia ya mkojo.

Ugonjwa huu huweza kumpata mtu yeyote pasipo kujali ni mwanaume au mwanamke. Hata hivyo, mwanaume huweza kuhisi dalili za UTI mapema zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na tofauti za kimaumbile.

Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria hupata urahisi wa kuingia ndani.

Chanzo cha UTI
Tatizo hili husababishwa na vyanzo mbalimbali, lakini zaidi maambukizi yanayosababisha tatizo hili ni bacteria au virus. Bakteria wanaosababisha UTI ni ‘e.coli’ na vijidudu vingine vya magonjwa ya zinaa mfano (klamidia) na vijidudu vya kisonono.

Virusi ambavyo husababisha tatizo hili ni kama vile ‘herpes simplex’ na ‘cytomegalo virus,’ sababu nyingine ni kuumia njia ya mkojo au kuwekewa mrija wa mkojo. Kemikali ni kama vile dawa za kuua mbegu za kiume au dawa za kupaka ukeni.
Kushiriki ngono na wanawake au wanaume wengi kwa upande wa wanawake pia ni mojawapo ya chanzo cha tatizo kwa kiasi kikubwa.

Wengine wanaopatwa zaidi na tatizo hili ni wale wenye tabia ya kufanya ngono au 
 kuwaingilia wengine kinyume na maumbile.

Dalili za UTI
Dalili zinazotofautiana kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume mwenye tatizo hili anaweza kukojoa mkojo wa njano sana kila wakati na unakuwa na harufu mbaya hata ukinywa maji mengi na wakati mwingine mkojo huambatana na damu.
Mwanaume anaweza kutokwa na manii au shahawa kwenye mkojo au anapojikamua haja kubwa, huhisi muwasho katika njia ya mkojo na ukiminya uume unahisi unauma na wakati mwingine unakuwa umevimba.

Uume ulegea au unaposimama huuma, vilevile hupata maumivu unapotoa manii wakati wa tendo, lakini manii huweza kuambatana na damu. 

Athari kubwa kwa wanaume ni kupungua nguvu za kiume na kuziba njia ya mkojo, Kwa wanawake hushambuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu na moto wakati wa kukojoa, homa za mara kwa mara na kutetemeka, wakati mwingine unaweza kuhisi malaria au taifodi, pia kila mtu mwenye UTI huisi kukojoa mara kwa mara ,pamoja na nyonga zote huuma na hutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na muwasho.  

Hata hivyo, ulaji wa tunda la tikiti maji kwa wingi huweza kusaidia sana kusafisha njia ya mkojo na kukusaidia kuondokana na tatizo hili la UTI. 

Kwa makala nyingine nyingi za afya hakikisha hukosi gazeti lako la TABIBU kila siku ya Alhamisi kwa shilingi 500/= tu.
 
Makala hii imeandaliwa na kuletwa kwenu na Mandai Harbalist Clinic, Kituo cha tiba asilia ya magonjwa sugu kilichopom jijini Dar es Salaam maeneo ya Mongolandege, Ukonga Mombasa. Au unaweza kuwasiliana nao kwa namba za simu; 0653 163 838 / 0752 163 838

No comments:

Post a Comment