- Daktari ajitokeza, asema anayo tiba asilia
- Ajinadi kutoa ofa kwa viongozi wa kitaifa kuwatibu bure
- Mashuhuda waliopona wajitokeza
Ugonjwa wa kisukari hujitokeza wakati ambapo
kongosho hushindwa kuzalisha insulini ya kutosha au wakati mwili unaposhindwa
kutumia insulini inayozalishwa kwa ufanisi. Insulini ni homoni inayosimamai kiwango
cha sukari katika damu.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takwimu
zinaonesha kuwa mnamo mwaka 2010 zaidi ya asilimia 80 ya vifo vya ugonjwa wa
kisukari vimekuwa vikitokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati, huku
wataalam wakisema kuwa, ifikapo mwaka 2030 idadi hiyo itaongezeka maradufu.
Sababu inayopelekea ugonjwa huu ni pamoja na mitindo
ya maisha isiyofaa hususani maisha ya kisasa hasa kwa waishio maeneo ya mijini.
Mitindo hiyo isiyofaa ni pamoja na aina ya vyakula vinavyoliwa, unywaji pombe
na uvutaji sigara uliokithiri pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili.
Inaelezwa kuwa mwaka 2004, watu milioni 347 duniani kote walikuwa na kisukari, huku wastani wa
watu milioni 3.4 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa huo.
Ugonjwa wa kisukari hutokea pale tezi kongosho (pancrease)
inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya insulini au mwili
unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulini na kusababisha
kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au kitaalam ‘hyperglycemia’.
Insulini ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na
kongosho ili kudhibiti sukari katika damu. Aidha, ugonjwa wa kisukari unaweza
kusababisha kuwa na kiwango kidogo cha insulini mwilini au mwili kutosikia
kichocheo hicho au yote mawili.
Ugonjwa huu huwaathiri watu wengi hata hapa nchini kwa
sasa, huku wengi wakionekana kujigundua na ugonjwa huu mara tu wanapoanza kuona
dalili kuu za kisukari, ambapo wengi huchelewa sana
kugundua. (Look for Tanzania statistics)
Aina
za kisukari
Aina ya kwanza ya kisukari (Type 1 - Diabetes
Mellitus). Hii ni aina ya ambayo huwaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii
hujitokeza pale ambapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zinakuwa zimekosekana
katika tezi kongosho au kuharibika kutokana na sababu yoyote ile, na hivyo
kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulini kwa njia ya sindano au pampu kila siku za maisha yao ili waweze kuishi. Kwa sababu hiyo,aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea insulini (Insulin Dependent Diabetes Mellitus) (IDDM).
Aina nyingine ya kisukari ni kisukari aina ya pili (Type
2 - Diabetes Mellitus). Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina
hii ya kisukari husababishwa na kupunguza utendaji kazi wa homoni ya insulin au
seli kushindwa kutumia insulini ipasavyo. Hali hii mara nyingi husababishwa na
unene uliopitiliza yaani ‘obesity,’
au hali ya kutoushughulisha kabisa mwili.
Katika aina hii ya kisukari, insulini huzalishwa kwa
kiwango cha kutosha, isipokuwa tatizo hujitokeza katika suala la ufanisi na
utendaji kazi wake na hii inamaanisha kwamba wagonjwa wa aina hii ya kisukari
huwa hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Aina hii hujulikana pia
kama kisukari kisichotegemea insulin (Non-Insulin Dependent Diabetes Mellitus).
Aina hii ya
kisukari huathiri karibu asilimia 2 hadi 5 ya mama wajawazito wote, ingawa
wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua. Hata
hivyo, wajawazito ambao hupata aina hii ya kisukari huweza kuendelea kuwa na
ugonjwa huo hata baada ya ujauzito na hatimaye kuwa na aina ya pili ya kisukari
maishani.
Visababishi
vya kisukari
·
Matumizi ya sukari nyingi na vyakula vya
mafuta
·
Kurithi kutoka kwa wazazi
·
Unywaji wa pombe wa kupindukia
·
Kutofanya mazoezi
·
Anasa na starehe na mtindo wa maisha
usiofaa
·
Kula vyakula vilivyotengenezwa kwa
kuongezewa sukari, hasa vyakula vya viwandani (processed foods) n.k.
Dalili
za kisukari
Kukojoa mara kwa mara, mgonjwa kuhisi kiu kali na
kunywa maji kwa kiwango cha kupitiliza, mgonjwa kuhisi njaa na kula mara kwa
mara, kuchoka haraka, mgonjwa kuwa na hasira, kupungua uwezo wa kufikiri pamoja
na kusikia njaa n.k.
Mbali na dalili hizo, mgonjwa pia huweza kupata
madhara ya muda mrefu, ambayo ni pamoja na kupata mtoto wa jicho na upofu,
magonjwa ya figo, kupata magonjwa ya kinywa na kung’oka kwa meno, mwili kufa
ganzi na kupoteza hisia hasa mikononi na miguuni, vidonda kutopona upesi na
hatari ya kukatwa mguu. Hata hivyo,
madhara haya ya muda mrefu huweza kuzuilika endapo mgonjwa atafuata masharti ya
wataalam wa afya hasa kuhusu chakula na mazoezi na maelekezo ya utumiaji sahihi
wa dawa au insulini.
Pia kuna hatari zaidi ya watu wanopatwa na kisukari kupatwa
na magonjwa ya moyo, kiharusi, kuharibika kwa kibofu cha mkojo, shinikizo la
juu la damu sambamba na ugonjwa wa fangasi.
Baada ya kufahamu hayo kuhusiana na ugonjwa huu wa
kisukari, blog ya gazeti hili la tabibu jumamosi hii itakuletea mashuda
waliopona pamoja na namna tiba asili inavyotibu na kumaliza kisukari. Hakikisha
hukosi muendelezo wa makala hii.
Gazeti lako la TABIBU wiki hii lipo mitaani na
unaweza kujipatia nakala yako kwa shilingi 500/= kila Alhamisi.
No comments:
Post a Comment