Karibu mpenzi msomaji
wetu wa blog ya gazeti la TABIBU katika safu hii ya kutoka Miracle Food Clinic.
Ambayo hupatikana ndani ya gazeti letu kila wiki Alhamisi, matumaini yangu u
mzima wa afya tele.
Kuna vyakula vingi
sana ambavyo vinaonekana kuvutia na kuwa na ladha nzuri mdomoni, lakini vita
kubwa hufanyika wakati wa uyeyusho na katika ufanyaji kazi mwilini. Kwa mfano,
mchanganyiko wa chumvi na kachumbari (salad) sio mzuri kiafya japokuwa una
ladha nzuri, chumvi hufanya kazi ya kufyonza maji ambayo huondoka na
virutubisho vyote unavyotegemea kuvipata kutoka kwenye kachumbari hiyo, hivyo
kachumbari hubaki kuwa haina kazi mwilini.
Pia mpenzi msomaji
unashauriwa kuepuka kuchanganya matunda machachu na matamu. Hii kwa ni sababu
matunda machachu hupunguza kasi ya uyeyusho wa haraka wa sukari ya matunda
matamu na kupelekea matunda matamu kuchacha.
Unaweza kujiuliza
mbona vyakula hivi vinavyosemekana kuwa mchanganyiko wake ni hatari tumekuwa
tukila kwa takribani maisha yetu yote bila athari? Jibu ni kwamba athari
iletwayo na sumu ya vyakula, madawa, hewa na nyinginezo hutofautiana katika
kutoa matokeo na kukujulisha kuwa unasumbuliwa na tatizo fulani. Hata hivyo,
kumekuwa na magonjwa mengi makubwa yanayosumbua watu wengi huku wakijiuliza
wamepata wapi athari hizo, kumbe ni mfumo uliojiwekea kwa kipindi kirefu na
sasa ndio matokeo yake.
Tukiangalia
mchanganyiko mwingine, tunakutana na kipengele cha vinywaji na vyakula vigumu,mfano
chai, kahawa, pombe na vinywaji laini ukichanganya na chakula kigumu, mfano wa
kitafunio, husababisha matatizo katika uyeyusho.
Pia epuka kula
vyakula vya mafuta na protini. Miongoni mwa vyakula vinavyopasa kuliwa peke
yake ni maziwa, tikiti (huyeyuka kwa urahisi kuliko tunda lolote na ni rahisi
kuchacha). Kuhusu vinywaji, ni kama sheria ilivyo, vinywaji havipaswi kuliwa na
vyakula vigumu. Kinywaji kina tabia ya kupita kwa kasi mpaka tumboni (utumbo)
na kuchukua vimeng’enyo vyote vya uyeyusho ambapo kitendo hicho huzuia uyeyusho
kufanya kazi nyingine.
Matunda yanatakiwa
yaliwe peke yake tena nusu saa kabla ya mlo kamili. Sukari pia huchukua ratiba
sawa na matunda.
Baada ya kueleza
hayo, mpenzi msomaji sasa tuangalie unawezaje kuboresha uyeyusho (tumboni).
· Kula pindi unapohisi
njaa, mwili unaweza kuvumilia matokeo yoyote ya hatari hata kama mchanganyiko
wa chakula sio mzuri endapo tu kama una njaa.
·
Fanya
mazoezi mepesi kwa afya ya tumbo lako na uyeyusho kwa ujumla.
· Kula chakula cha aina
moja au kiasi kwa wakati. Vyakula vya aina nyingi huleta shida katika tumbo na
uyeyusho kwa ujumla wakati tumbo linaweza kuvumilia aina moja ya chakula au
chakula kiasi. Hivyo basi, ulaji wa vyakula vingi huvifanya visubiriane katika
uyeyusho na hicho sio kitu sahihi kiafya.
Kuwa na tabia ya kula
vyakula vibichi kama matunda na karanga.
Kwa haya na mengine
mengi usikose kufuatilia gazeti la TABIBU kila siku ya Alhamis
Kwa makala hizi na
nyingine nyingi za kuelimisha kuhusu Afya, hakikisha hukosi kopi ya gazeti lako
la TABIBU kila wiki siku ya Alhamis.
No comments:
Post a Comment