Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Wednesday, August 27, 2014

Chungwa: tiba ya kuzibua mirija


Habari mpenzi msomaji wa blog ya gazeti la TABIBU, ni matumaini yangu mzima wa afya. Karibu tena katika safu hii kutoka Miracle Food, ambayo hupatikana kila siku ya Alhamisi katika gazeti la TABIBU, kama ilivyokawaida wajibu wetu ni kukupa elimu ya afya na vyakula mbalimbali. Leo tumekuandalia chungwa kama tiba ya magonjwa mbalimbali lakini hasa kuzibua mirija ya uzazi kwa wanawake.

Pamoja na uwepo wa maradhi mengi ya mfumo wa uzazi wa akina mama kama kutokwa na damu nyingi au kidogo wakati wa hedhi, maumivu wakati wa hedhi au wakati wa tendo, tatizo la mayai kutopevuka kwa wakati nk. Lakini hasa tutakachokiangalia leo ni kuziba kwa mirija ya uzazi.

Chungwa ni tunda linalostawi ulimwenguni kote, lakini haswa lilianzia kusini mwa bara la Asia, huku likilimwa sana huko nchini China.

Miaka ya nyuma sana mnamo 2500 BC (kabla ya kristo) chungwa limekuwa likiitwa tufaa la kichina, baada ya hapo watu wakalieneza Uingereza na Marekani katika miaka ya 1500. Hata hivyo mnamo mwaka 1897 tunda hili likatambulika ulimwenguni kote. Tunda hili huweza kuliwa likiwa katika hali ya uhalisia (fresh) au kwa kutengeneza juisi.

Kwa kawaida chungwa limekuwa likisifika kwa uwingi wa vitami C, lakini kwa sasa imegundulika licha ya kuwa na vitamin C pia lina zaidi ya ‘phytochemicals’ 170, ambazo husaidia ufanyaji kazi wa vitamin mwilini. Ingawaje wataalam wanasema kuwa vitamin C inayopatika kwa ulaji wa chungwa inaweza kuwa na kiasi kikubwa zaidi ya kinachohitajika mwilini hivyo ni hatari, kwa hiyo huwa wanashauri ni vyema kupata vidonge vya vitamin hospitali.



Chungwa lina sehemu kuu tatu nazo ni
 Ganda (exocarp): hili eneo la nje kabisa ambalo lina mafuta ya muhimu yenye ‘flavonoids.’ Ganda la chungwa hutumika kulinda mfumo wa misuli na kuongeza hamu ya kula na kutuliza mishipa ya fahamu.

Ganda jeupe la ndani (mesocarp) : hili ni eneo la ndani ambalo huonekana baada ya chungwa kumenywa, ganda hili jeupe lina ‘pectin,’ ambayo ni aina ya nyuzinyuzi (fibre) zipatikazo kwenye mbogamboga. kazi yake ni kuzuia lehemu (cholesterol) na kansa, ni vyema kuthamini afya yako kwa kutolitupa ganda jeupe la chungwa ingawa halina ladha nzuri ya kukuvutia lakini ni vyema ule.

Endocarp: (Juicy Pulp): hili ni eneo la ndani ambalo ndio hutoa juisi, watu wengi hukimbilia hapa, limetengwa kwa vyumba vyumba vipatavyo 8 mpaka 12 ambamo kuna chembe (cell) ndogondogo zenye maji ya matunda (Juice). Mistari hii iliyotenganisha vyumba hivi, baada ya kuwa maji ya tunda yameshakamuliwa bado ina kiasi cha ‘pectin’ kama (fibre) nyuzinyuzi za

Aina nyingine za mbogamboga.
Tofauti ya tunda na (Juice) maji yake ni kwamba unapokunywa juisi unapata virutubisho sawa kwa njia rahisi, lakini ‘calcium’ na ‘fibre’ inakosekana ambayo hupatikana kwenye ulapo tunda lenyewe. Wakati wa utengenezaji au uandaaji wa juisi ya chungwa vitamin C hupotea kwa asilimia 10. Virutubisho vilivyobaki huwa kama vilivyo na haswa juisi ilitiwa ubaridi wa jokofu na hata kuganda ni nzuri zaidi.

Inaaminiwa kuwa kula machungwa manne kwa siku ni kinga sahihi kwa wale wanaohitaji kinga ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Mpenzi msomaji wa blog hii ya TABIBU hadi kufikia hapo ndio mwisho wa somo letu la machungwa kwa kutumia kama tiba ya kuzibua mirija ya uzazi na maradhi mengineyo, tukutane tena wiki ijayo katika mfululizo wa masomo mengine ndani ya gazeti la TABIBU kila siku ya Alhamisi kwa shilingi 500/= tu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Miracle Food Clinic & Counseling kwa simu namba 0755 093 418, 0715 093 418 na 0688 063 418. Tupo Kariakoo mtaa wa msimbazi jengo la Klabu ya Simba ghorofa ya tatu. Karibuni


4 comments:

  1. Huu ubabaishaji sasa, mbona hamjataja kuhusiana na chungwa kuzibua mirija

    ReplyDelete
  2. Dr kanyas mtaalamu wa tiba asili anazo daww kwa ajili ya ugumba..utasa
    .hedhi isiyo na mpangilio...pia anazo dawa za ngugu za kiume ....pia anazo za kurefusha uume na kunenepesha uume...mtafute kupitia 0764839091

    ReplyDelete