Na:Edger Kapagi
Kwa
maoni yangu, mhindi ni mmea wenye utaratibu wa kuvutia, kuanzia majani yake
hadi kwenye mbegu zilizo kwenye hindi lenyewe. Kila kitu kimepangwa kwa
mpangilio wenye kupendeza. Isitoshe, mmea huu unapokuwa ‘unazungumza’nawe. Unakuambia
ikiwa una kiu au hauna lishe ya kutosha.
Kwa
kawaida mtoto wa kibinadamu hulia anapohitaji kitu. Kama tu mmea mwingine, mhind
nao hutoa ishara zinazoonekana kama vile kubadili rangi na umbo la majani yake,
ili kueleza mahitaji yake, hivyo unahitaji kuelewa ishara hizo. Huenda majani
yenye rangi nyekundu ya zambarau yakaonesha kwamba mhindi hauna fosfati, pia dalili
nyingine zinaweza kuonesha ukosefu wa magnesi, nitrojeni au potashi. Hivyo
mkulima anapoungalia anaweza kutambua ikiwa mhindi wake una ugonjwa au
umeathiriwa na kemikali.
Mhindi
ulianza kukuzwa huko America, huenda katika nchi ya Mexico na kuenea
ulimwenguni kote. Waperu walioishi kabla ya enzi ya wainka waliabudu mungu wa
kike wa mahindi aliepambwa kwa taji lililotengenezwa kwa bunzi za Mhindi. Bunzi
hizo zilitokea kichwani mwake kama nyaya katika gurudumu.
Hata
hivyo, wakaaji wa ulaya waligundua mhindi mnamo 1492, baada ya mvumbuzi Christopher Columbus kuwasili katika visiwa vya
karibea.
Kuna
aina nyingi za mahindi yanayogawanywa katika makundi sita makuu: dent, flint, flour,
sweet, waxy na Pop corn. Mahindi aina ya sweet hayakuzwi sana kama aina
nyingine. Utamu unaopatikana katika aina hii ya mahindi unatokana na kasoro fulani
ambayo huizuia kubadili kiasi cha kutosha cha sukari kuwa wanga. Zaidi ya
asilimia 60 ya mahindi yanayokuzwa ulimwenguni hutumiwa kulisha mifugo, huku
asilimia 20 hivi ikilisha wanadamu. Asilimia inayobaki hutumiwa viwandani au
kama mbegu.
Huko
India huita CORN(makai) na America (Indian corn) haya mahindi ni ya njano
mengine ya kawaida na mengine ya bisi (Popcorn), haya ndiyo nitaelezea umuhimu
wake katika afya zetu.
Haya
mahindi ya njano endapo yatatumika vizuri yanapunguza kuongezeka uzito (weight
gain), mahindi haya yana magnesium kwa wingi yanayosaidia matumbo yetu yawe
vizuri (wonderful bowel regulator). Yanasaidia kujenga mifupa na misuli, yana
phosphorus kwa wingi inayosaidia kujenga ubongo vizuri na mfumo wa fahamu,
huimarisha kuimarisha nguvu za uzazi, kupunguza lehemu kwenye damu (blood
cholesterol level), kuondoa chunusi usoni, zaidi ni kwamba mahindi ya njano
yanapochanganywa na soya, ulezi, karanga na Drumstick (mlonge) hufaa sana kwa
utapiamlo na HIV/UKIMWI.
Kwa
upande wa bisi husafisha meno, huimarisha nguvu za uzazi, kupunguza sukari
mwilini, kisukari, kusafisha damu, pia watu wengine na waathirika wa UKIMWI
wazitumie kuboresha afya.
Mhindi
una kitu kimoja kinaitwa ndevu za mahindi, ndefu hizi zinafaida kubwa kwa
binadamu, kwani zina potassium nyingi ambazo zinasaidia kutibu magonjwa yafuatayo; kwa wanaokojoa kitandani, maumivu
ya prostate, maumivu ya mfumo wa mkojo (UTI), mawe kwenye figo, moyo
kutokufanya kazi yake vizuri (congestive heart failure), kisukari ukichanganya
na Drumstick, uchovu, BP (Hbp), kupunguza lehemu(cholesterol)nk.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia, ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya
ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali
ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali
wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia),
kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause),
kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo,
kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si
rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Kadri
mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua tatizo analokuwa nalo na
anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Je waweza kukoboa mahindi haya ya njano kwaajili ya ugali na je husaidia vidonda vya tumbo?
ReplyDelete