Chicago, Marekani
Tafiti
zinasema kuwa mafuta ya samaki aina ya Omega-3 yanaweza kusaidia ubongo
kutokana na matatizo yanayosababishwa na pombe kwa asilimia 90.
Watafiti
wamegundua kwamba seli za ubongo zilizohusishwa na kiasi kikubwa cha pombe
ziliweza kulindwa zisiharibike na hatimaye kufa kwa mkusanyiko unaopatikana
katika mafuta ya samaki.
“Mafuta
ya samaki yana uwezo wa kusaidia kuutunza uwezo wa ubongo katika matumizi
mabaya kabisa ya pombe,” alisema mtafiti Michael Collins kutoka Shule ya Madawa
ya Chuo Kikuu cha Loyola, Chicago Marekani.
Katika
utafiti huo, Collins na wenzake waliweka ubongo wa panya katika kiwango cha
pombe kinachozidi mara nne ya kiwango kinachoruhusiwa kisheria kwa waendesha
magari, kiasi cha pombe ambacho huwa kinaonekana kwa wanywaji pombe
waliokubuhu.
Tabia
za ubongo huo ziliweza kulinganishwa na tabia za mkusanyiko huo huo wa ubongo
uliowekwa pamoja na omega-3 “docosahexaenoic
acid” (DHA) kutoka katika mafuta ya samaki.
Aidha,
watafiti wamegundua kulikuwa na asilimia 90 ya upungufu ya ‘neuro-inflammation’
na kifo cha nuroni katika seli za ubongo zilizowekwa kwenye pombe na (DHA)
kuliko zile seli zilizowekwa kwenye pombe peke yake.
“Pombe
katika kiwango cha kawaida inaharibu seli na hivyo kuzifanya kuwa sugu na kuendana
na matatizo makubwa yanayoweza kusababisha mzio. Lakini kiasi kikubwa cha pombe
kinaharibu zaidi seli na kupelekea kuua seli na kusababisha ‘neuro-inflammation’,”
alisema Collins.
Kulingana
na watafiti, wanasema kuwa, haina maana kwamba watu watumie mafuta ya samaki halafu
baada ya hapo waendelee kutumia pombe vibaya kwani hakuna manufaa watapata kwa
njia hiyo.
Kwa
habari kama hizi na nyingine nyingi hakikisha unapata nakala ya gazeti lako la
TABIBU kila siku ya Alhamisi kwa shilingi 500/= tu
No comments:
Post a Comment