KIHARUSI
KINATIBIKA
Na Juma Diwani
Kiharusi
au kwa jina la kitaalam ‘stroke’, ni
mojawapo ya magonjwa yasiyoambukiza yanayotisha kwa binadamu. Ugonjwa huu
huleta kupooza kwa viungo vya mwili vya binadamu na husababishwa na kuzibwa au
kupasuka kwa mishipa inayopeleka damu katika ubongo na hatimaye seli za ubongo
kufa kutokana na kukosa hewa ya oksijeni na lishe ya kawaida.
Kiharusi
ni hali ya dharura ambayo hupelekea watu wengi kuwa nadhana ya uchawi wakati
wanapatwa na tatizo hilo kwani linaweza kutokea mahala popote na wakati wowote.
Aina za Kiharusi
Gazeti
hili lilimtafuta Dk. Auson S. Rwehumbiza ambaye ni Mratibu wa Kisukari katika
Kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza. Alisema kuwa tatizo hili linawasumbua watu
wengi na zipo aina nyingi za kiharusi kulingana na wapi tatizo la kupooza
hutokea. Rwehumbiza alifafanua miongoni mwa aina hizo kuwa ni:
1.
Kiharusi
cha kukosa hewa kwenye ubongo (Ischemic
stroke)
Aina
hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo
hupungua na kusababisha tishu za ubongo za eneo lililoathirika kushindwa
kufanya kazi zake vizuri.
Tatizo
hili hutokea baada ya mshipa wa ateri kuziba kutokana na kuganda kwa damu, hali
ambayo inasababisha damu isisafiri vyema na kuelekea kwenye ubongo.
2.
Kiharusi cha kuvuja damu ndani ya ubongo (Haemorrhagic stroke)
Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya
damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu ubongoni (cerebral hemorrhage). Mara nyingi aina
hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia
ya ajali ya kichwa.
Sababu zinazopeleka kiharusi
Kuna
sababu nyingi zinazopelekea mtu kupatwa na ugonjwa wa kiharusi. Miongoni mwa
sababu hizo ni;
I.
Mishipa
ya damu kuzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwilini, hali inayoitwa
kitaalam kama ‘atherosclerotic plaque’
na hatimaye damu huganda katika mishipa.
II.
Shinikizo
la damu la muda mrefu lisilothibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa
midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo.
III.
Kuganda kwa chembechembe nyekundu za
damu za mgojwa wa ‘sickle cell’ kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu
hivyo kusababisha kiharusi.
IV.
Kutofanya
mazoezi (mazoezi rafiki)
V.
Kunywa
pombe, uvutaji wa sigara na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Dalili za kiharusi
Dk.
Rwehumbiza alibainisha dalili zinazoweza kutumika kumtambua mtu anayesumbuliwa
au anaelekea kupatwa na kiharusi, ambazo ni;
· Kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake.
· Kupungua kwa ufahamu wa
hisia.
· Kutokwa na mkojo bila
kujijua.
· Kupoteza uwezo wa
kuongea, kusikia na kula au kunywa.
· Ukosefu wa kumbukumbu
· Madiliko ya upumuaji na
kiwango cha moyo kudunda.
Tiba ya Kiharusi
Kwa mujibu wa Dk.
Rwehumbiza, alisema kuwa miongoni mwa tiba ya kiharusi kwanza ni kutambua
tatizo hilo limetokana na nini, kufanya mazoezi, kumeza ‘Junior aspirin’,
kumeza virutubisho vya vitamini B pamoja na kuthibiti magonjwa sababishi kama
kisukari na presha.
Angalizo: Usitumie dawa yoyote bila kupima na kufuata
ushauri
Shirika la Afya Duniani linasemaje
Kila ifikapo tarehe 29
ya mwezi wa 10 kila mwaka, nchi zote huadhimisha Siku ya Kiharusi. Hata hivyo,
shirika hilo linaeleza kuwa tatizo hili ni mojawapo ya magonjwa yanayoongoza
kusababisha vifo duniani.
Inakadiriwa kuwa watu
zaidi ya milioni 5 duniani walifariki kutokana na kiharusi mwaka 2005 na
asilimia 85 ya vifo hivyo vilitokea katika nchi zenye kipato kidogo na cha
kati.
Watu walio katika hatari zaidi ya kupatwa na kiharusi
TABIBU lilimtafuta Dk. Herbert
Mngoma kutoka katika Hospitali ya Hindu Mandal ambaye alifafanua juu ya watu
waliokuwa katika hatari ya kupatwa na tatizo hilo.
Alisema kuwa, watu walio na
umri kuanzia miaka 40, wenye matatizo ya presha, kisukari na magonjwa ya moyo
wapo katika hatari zaidi ya kupatwa na kiharusi.
Aliongeza kwa kusema
kuwa watu walio na matatizo ya kisukari na presha na wakaacha kutumia dawa, nao
wapo katika hatari zaidi ya kupatwa na kiharusi.
Vijana
pia wapo katika hatari zaidi ya kupata kiharusi kutokana na tafiti zilizofanywa
na ‘The Lancet Medical Journal’ za hivi karibuni. Tafiti hizi zilionesha kuwa
zaidi ya watu 83,000 walio na umri wa miaka 20 na chini duniani wanapatwa
na kiharusi.
Hata
hivyo, imeelezwa kuwa ifikapo mwaka 2030, vifo vinavyotokana na kiharusi
vitakuwa mara mbili zaidi ya sasa.
Jinsi ya kuepukana na kiharusi
Dk. Mngoma alisema kuwa
kuna njia mbali mbali za kuepukana na tatizo hilo linalowasumbua watu wengi.
· Kwenda kupima afya zetu
mara kwa mara
· Kuwa na tabia ya kufanya
mazoezi angalau kwa dakika 30 kila siku.
· Kuacha kuvuta sigara
· Kutumia chumvi na sukari
kwa kiasi
· Kutumia mafuta ya mimea
· Kuthibiti kisukari
Hata hivyo, Dk.Mngoma
ameiomba serikali itoe elimu ya kutosha kuhusu tatizo hilo kwani ni hatari na
linawapata watu wengi kwa sababu nyingine zinazozuilika.
“Serikali kupitia Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii ikitoa elimu ya kutosha kuhusu kiharusi kwa kina
itawafikia watu wengi.”
Wataalam wa Tiba asilia wanasemaje
Gazeti hili lilimtafuta
mtaalam wa tiba asilia Dk. Esibon N. Baroshigwa wa Amani Sanitarium Clinic iliyopo
Dar es Salaam ambaye alisema kuwa watu wengi wanasumbuliwa na kiharusi kwa muda
mrefu bila kupona lakini tatizo hili linatibika kwa njia mbadala.
Hata hivyo, Dk.
Baroshigwa alisema kuwa miongoni mwa dawa zinazoweza kutibu tatizo hilo ni ‘Brain
Activator’ na ‘OP’-Juisi ya matunda maalum ambazo zinapatikana
katika kituo chake na mgonjwa anaweza kupona ndani ya mwezi mmoja.
Watu maarufu waliowahi kuugua kiharusi
Kwa mujibu wa mitandao
mbalimbali, imeelezwa kuwa miongoni mwa watu waliowahi kuugua ugonjwa wa
kiharusi ni pamoja Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999.
Kifo cha Mwalimu Nyerere
kinasemekana kuwa hakikusababishwa na kiharusi bali kilitokana na ugonjwa wa saratani
ya damu.
Wengine wanaosadikika
kuugua ugonjwa huo ni pamoja msanii nguli wa maigizo, Said Ngamba maarufu kama ‘Mzee
Small’ ambaye alifariki dunia mwaka huu.
Mwanasiasa maarufu
aliyeishi nchini Urusi, Vladimir
‘Lenin’ Ilyich
aliyefariki dunia mwaka 1924, alipatwa na kiharusi mara tatu maishani mwake.
Matatizo yatokanayo na kiharusi ndiyo yaliyomuua. Rais wa 28 wa Marekani,
Woodrow Wilson pia alifariki baada ya kuugua kiharusi cha ghafla. Wapo watu
wengine wengi maarufu waliougua kiharusi ingawa alikuwa na
ugonjwa wa saratani ya damu ambayo nayo huenda ilisababisha kifo chake.
Watanzania wanasemaje kuhusu tatizo hilo
TABIBU lilifanya
mahojiano na Watanzania 20 ambao walisema kuwa kiharusi ni ugonjwa hatari
unaowasumbua watu wengi na kuiomba Serikali kupitia wizara husika kutoa elimu
ya kutosha kwa Watanzania.