Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Tuesday, December 16, 2014


Kuvimba kwa tezi dume (Prostatitis)
Ni ile hali ya tezi dume kuathirika kutokana na vyanzo mbalimbali mfano, bakteria n. Kuathirika kwa hii tezi dume kunaweza sababisha hata utendaji kazi wake kupungua na inapatikana chini ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kuzalisha manii kwa ajili ya kurutubisha na kusafirisha mbegu za kiume kutoka kwenye korodani. Tatizo hili linawaathiri wanaume bila kujali rika lakini wanaume kuanzia miaka 50 wameonekana kuathirika zaidi na hili tatizo


Chanzo cha tatizo
Chanzo kikubwa cha ‘prostatitis’ ni kushambuliwa kwa tezi dume na bakteria mbalimbali ambao wanaweza kuwa ni visababishi vya magonjwa mbalimbali ya zinaa; mfano kaswende, kisonono, pangusa n.k au bakteria wanaoshambulia mfumo wa mkojo (UTI) wanaweza kupenya na kuifikia tezi dume na kuishambulia. Vyanzo vingine ni kushuka kwa kinga za mwili na ajali zinazopelekea kuumia katika eneo ambalo tezi dume ipo. Pia kuna mazingira hatarishi yanayopelekea mwanaume kuathirika na hili tatizo;
·      Kama mwanaume alishawahi kuwa na hili tatizo na hakupata matibabu sahihi
·      Kuwa na maambukizi katika kibofu cha mkojo au mrija unaotiririsha mkojo (urethra)
·      Kutokunywa maji mengi
·      Kuwa na wapenzi wengi na kushiriki tendo la ndoa na mpenzi mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa na VVU/UKIMWI.

Dalili za hili tatizo
·  Maumivu wakati wa kutoa haja ndogo au kuhisi kama mkojo ni wa moto na maumivu wakati wa kufika kileleni
·      Kwenda haja ndogo mara kwa mara
·      Mtiririko wa mkojo kuwa dhaifu
·      Maumivu chini ya kitovu
·      Maumivu ya kiuno na chini ya mgongo
·    Maumivu ya sehemu ambayo ipo katikati ya korodani na sehemu ya kutolea choo kubwa
·      Maumivu ya korodani na uume
·      Mwanaume mwenye tatizo hili anaweza akawa na homa

Madhara endapo matibabu yatachelewa
·      Kusambaa kwa bakteria mbalimbali katika damu (bacteremia)
·      Kuwa na jipu kwenye tezi dume (prostatic abscess)
·      Ugumba kutokana na kuathirika kwa manii, mbegu za kiume
·      Pia tatizo hili linaweza likasababisha kansa ya tezi dume (prostate cancer)

No comments:

Post a Comment