Utagunduaje maabukizi kwenye
uzazi (Diagnosis of PID)
Na Dk. Fadhily Emily
Kama tulivyokwisha katika
makala zilizopita katika safu hii dalili za maambukizi kwenye viungo vya uzazi
kwa mwanamke kama vile kutokwa uchafu sehemu za siri, homa, maumivu chini ya
kitovu, kutokwa na hedhi bila mpangilio,
maumivu wakati wa tendo la ndoa na maumivu wakati wa kutoka hedhi na nyinginezo, hivyo basi ili kugundua ugonjwa wa PID ni lazima kuchukua historia vizuri ya mgonjwa.
maumivu wakati wa tendo la ndoa na maumivu wakati wa kutoka hedhi na nyinginezo, hivyo basi ili kugundua ugonjwa wa PID ni lazima kuchukua historia vizuri ya mgonjwa.
Daktari atampima tumbo mama
ili kugundua maumivu ya tumbo kama yapo sehemu gani na pia kufanyia vipimo kama
vile kupima uchafu kutoka ukeni na vipimo vingine kama Ultrasound.
Magonjwa mengine yanayofanana
na PID ni kama vile kidole tumbo (appenditis),
mimba kutunga nje ya mji wa mimba hasa ikitungwa kwenye mirija na kupasuka (ruptured actopic pregnance), kupasuka
uvimbe kwenye mfuko wa mayai (reptured
ovarian mass) au maambukizi ya vidudu kwenye mkojo (urinary tract
infection).
Madhara ya PID
Madhara ya haraka (immediate complication) ni magonjwa
yanayoweza kusababishwa na maambukizi kwenye mji wa mimba, vijidudu huweza
kusambaa na kuingia kwenye utumbo (peritonitis)
au wadudu kuingia kwenye mfuko wa damu (septichemia)
ambapo huweza kuathiri viungo kama magoti na mgonjwa kupata ugonjwa wa arthritis
na moyo (myocarditis).
Madhara ya muda mrefu ni kama
maumivu wakati wa tendo la ndoa (Dyspareunia),
kukosa kupata mimba (Infertility),
maambukizi kuwa sugu (chronic
imflammatory diseases) na uwezekano wa mimba kutunga nje ya mji wa mimba
yaani ectopic pregnance.
Matibabu
Mgonjwa atapatiwa tiba kwa muda usiopungua
siku 14 dawa zinazotumika ni kama levoflaxacin ikichanganywa na metronidozole.
Pia dawa zingine kama cefriaxone, dnycyline hutumika kwa
kipindi cha siku 14.
Matibabu haya hutumika kwa
wagonjwa wa nje (out patient),
wagonjwa watahitaji kuonwa na daktari baada ya siku 2 baada
No comments:
Post a Comment