Maajabu
ya ‘Good Luck Plant’
Na
Dk. Edger Kapagi
Mmea huu hupandwa sana na watu wengi kama maua hapa nchini
Tanzania.
Mmea huu una majina mengi katika nchi za Java, Fiji, Malaysia,
Indonesia, Samoa, Hawaii, Sumatra na New Guinea, nk.
Jina la kibotania huitwa ‘Cordyline Terminals’ na majina mengine ni ‘cordyline fluctiosa’, ‘ti plant’, Hawaiian good-luck plant’, ‘false
palm’, ‘canade indio’, ‘croto’, ‘keulenlilie’ na ‘red tree of
kings’. Waingereza huuita ‘goodluck
plant’. Mmea huu hukua hadi kufikia kimo cha mita 1 hadi 3 kufuatana na
mazingira ya nchi yalivyo.Mmea huu huwa na rangi ya zambarau au nyekundu kufuatana na
mazingira yalivyo.
Aidha, mmea huu hutumika kutibu magonjwa kama damu inayotoka
pamoja na mkojo, damu inayotoka kwenye ‘piles’,
kuzuia mimba zinazotoka kabla ya wakati wake, homa, pumu, kuumwa kichwa, kubana
kifua, maumivu ya mgongo, kuungua na moto, bawasiri, matende, jongo, uvimbe wa ‘scrotum’,
mafua, kikohozi, kifaduro, ‘gastritis’,
macho kuuma, fizi zinazotoa usaha, uvimbe unaotokana na kuteguka, ‘gingivitis’,
meno kuuma, kipara, mzio, maumivu ya tumbo, ‘enteritis bacillary dysentery’,
maumivu ya mifupa yanayotokana na baridi yabisi, maumivu ya sikio na koo.
Kinachotumika ni majani mabichi gramu 60 - 90, mizizi
iliyokaushwa gramu 30 - 60 na maua yaliyokushwa gramu 9 - 15 kwa kuchemsha
pamoja na maji.
Majani yanachanganywa na mafuta ya mbogamboga au mzeituni
kwa kutibu vidonda.
Hapa Tanzania, watu wengi hupanda mmea huu kwenye nyumba zao
kama maua wakiamini kuwa ni mmea wenye kuleta bahati na kufukuza pepo wabaya,
hupanda kwenye varanda au upenuni mwa nyumba.
Nchini Hawaii, watu hutumia mmea kwenye sherehe mbalimbali
kama kuleta baraka, utakaso na kufukuza laana nk.
Huko Java, wenyeji hula majani machanga kama mboga.
No comments:
Post a Comment