Fahamu kuhusu
ugonjwa wa Kaswende - 1
Na Abdallah Juma
Ugonjwa
wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya
‘Treponema pallidum’.
Ugonjwa
huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara
mengi.
Maambukizi
ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara mengi sana kama vile kujifungua
kiumbe ambacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa,
mtoto kupata matatizo wakati wa ukuaji wake, degedege na kuongezeka
kwa vifo vya watoto wachanga.
Ugonjwa
wa kaswende huathiri zaidi ya mimba milioni moja duniani kote kila mwaka
na kuchangia theluthi mbili ya vifo vya watoto wanaozaliwa wakiwa tayari
wameshakufa katika nchi za maeneo ya chini ya Jangwa la Sahara. Asilimia
30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende huishia watoto kufariki wakati wa
kuzaliwa.
Pia
asilimia nyingine 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende husababisha watoto
wanaozaliwa na ugonjwa huu kupata matatizo ya ukuaji, degedege na kuongezeka
vifo vya watoto kwa asilimia 50.
Kwa mfano,
Taasisi ya kudhibiti Ugonjwa wa UKIMWI nchini Tanzania (Tanzania National
AIDS Control Programme) au NACP katika ripoti yake ya utafiti
uliofanywa chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini ilitangaza
kuwa, maambukizi yote ya kaswende wakati wa ujauzito Tanzania bara kati ya
mwaka 2003 hadi 2004 yaliongezeka kwa wastani wa asilimia 6.7 kwa ujumla,
kuanzia mkoani Kilimanjaro ambako maambukizi yalikuwa ya asilimia 0.4 hadi
mkoani Tabora ambako yalikuwa ya asilimia 32.
Magonjwa
ya UKIMWI na kaswende mara nyingi huambatana pamoja ambapo pia ugonjwa wa zinaa
wa kaswende huongeza uwezekano wa mtu kupata UKIMWI.
Je, ugonjwa wa
kaswende huambukizwa kwa njia gani?
Kama
tulivyosema awali, kaswende husababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum.
Miongoni mwa njia za ugonjwa huu nipamoja na
· Kupitia kujamiiana bila kutumia
kinga au ngono zembe na mtu aliyeambukizwa kaswende.
· Mama aliyepata ugonjwa wa kaswende
wakati wa ujauzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.
· Kuambukizwa kupitia michibuko au mipasuko
kwenye ngozi wakati wa kujamiiana au wakati mwingine pale mtu anapogusana na
mtu mwenye kaswende ikiwa wote wawili wana mipasuko kwenye sehemu mbalimbali za
ngozi zao.
Sio
rahisi mtu kutambua kama ana michibuko au la kwenye ngozi kwani mingine huwa
midogo sana isipokuwa ile inayoweza kuonekana kwa macho, lakini huweza kuwa
njia ya maambukizo.
Dalili na viashiria
vya tatizo hili
Dalili na
viashiria vya ugonjwa wa kaswende hutegemea aina ya ugonjwa wa kaswende
wenyewe.
Kuna aina
tano za ugonjwa wa kaswende ambazo ni;
§ Ugonjwa wa kaswende wa
awali (Primary syphilis)
§ Ugonjwa wa kaswende
wa pili (Secondary syphillis)
§ Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
§ Kaswende ya baadaye
(Tertiary syphilis). Itaendelea.............
No comments:
Post a Comment