Dalili
za tatizo la kutopata ujauzito
Tatizo la kutofanikiwa kupata ujauzito kwa mwanamke linahusiana
moja kwa moja na kuwepo na tatizo kwa mwanaume.
Unaweza kusema kama una tatizo hili endapo unaishi katika
mahusiano ya kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna
mafanikio.
Ili mwanamke apate mimba ni lazima awe na sifa za kupata
ujauzito, na ili mwanaume aweze kumpa mwanamke mimba ni lazima awe na sifa za
kumpa mwanamke mimba. Matatizo haya yapo kwa pande zote mbili.
Wakati wa kutafuta ujauzito, ni vema mwanamke na mwanaume
washirikiane kwani mwanaume unaweza kujiona huna tatizo kumbe ukija kupima mbegu
zako utajikuta una tatizo kubwa.
Matatizo kwa mwanamke
Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo haya yafuatayo;
Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo haya yafuatayo;
- Atakuwa
amekaa na mume au yupo katika mahusiano ya kutafuta mtoto kwa zaidi ya mwaka
lakini hakuna mafanikio. Hulalamika maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara au
yanaweza yasiwepo, maumivu ya hedhi, kuvurugika mzunguko na kutoona ute wa
uzazi.
- Wengine
hawana hamu ya tendo la ndoa au kutojihisi raha wakati wa tendo, maumivu wakati
wa tendo au kutokwa na uchafu ukeni wakati mwingine huambatana na muwasho na
harufu.
- Anakuwa na
historia aidha ya kutumia njia za uzazi wa mpango, kuharibu au kutoa mimba,
historia ya kuzaa, au kufanyiwa upasuaji wa aidha uzazi au mirija. Ingawa
wengine hawana historia hizi.
Nini cha kufanya?
Endapo utahisi una matatizo ya kutopata ujauzito na unazo dalili
kama hizo hapo juu au huna, basi ni vizuri umuone daktari wa magonjwa ya
matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa. Uchunguzi utafanyika kuangalia
mfumo wako wa homoni au vichocheo vya uzazi, vipimo vya kizazi na mirija na
vingine ambavyo daktari atashauri. Uchunguzi na matibabu huchukua muda mrefu,
ni vema kufuatilia kwa makini.
Athari kubwa zinazotokea mara nyingi katika uzazi kwa mwanamke
ni kuziba kwa mirija ya mayai.
Mvurugiko wa mfumo wa homoni, matatizo ndani ya kizazi ambayo yanaweza kuwa uvimbe au maambukizi. Uwezekano wa kutibiwa na kufanikiwa upo endapo utazingatia.
Mvurugiko wa mfumo wa homoni, matatizo ndani ya kizazi ambayo yanaweza kuwa uvimbe au maambukizi. Uwezekano wa kutibiwa na kufanikiwa upo endapo utazingatia.
Matatizo ya uzazi kwa mwanaume
Mwanaume kama atazingatia uchunguzi na tiba naye anaweza
kufanikiwa ingawa akigundulika kama ana tatizo, tiba yake huchukua muda mrefu.
Uchunguzi wa mwanaume ni kuangalia mbegu za uzazi na kupima
korodani. Mwanaume unaweza kujifahamu kama una tatizo endapo utakuwa na dalili
zifuatazo; siyo lazima zote lakini mojawapo:
- upungufu
wa nguvu za kiume,
- kuishi na
mwanamke zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mimba,
- kutoa
manii nyepesi sana na zenye harufu mbaya,
- manii
nyepesi hutoka mara moja ukeni unapomaliza tu tendo la ndoa,
- maumivu ya
muda mrefu ya korodani, maumivu ya kiuno,
- maambukizi
ya mkojo ya mara kwa mara,
- uvutaji wa
sigara kwa muda mrefu,
- unywaji wa
pombe kali, na matumizi ya madawa ya kulevya mfano bangi na mirungi na
mengineyo.
Nini cha kufanya?
Matatizo haya hutibika kwa daktari wa matatizo ya uzazi kwenye hospitali. Vipimo vya mbegu za uzazi vitafanyika kuangalia kiwango cha mbegu na ubora wake kama zina uwezo wa kutungisha mimba.
Matatizo haya hutibika kwa daktari wa matatizo ya uzazi kwenye hospitali. Vipimo vya mbegu za uzazi vitafanyika kuangalia kiwango cha mbegu na ubora wake kama zina uwezo wa kutungisha mimba.
Vipimo vingine itategemea na uwepo wa matatizo mengine ya uzazi
kwa mwanaume kama kuwahi kumaliza tendo la ndoa, kushindwa kufanya tendo la
ndoa, upungufu wa nguvu za kiume, uchovu mkali baada ya tendo la ndoa, maumivu
ya kiuno, korodani na maumivu ya njia ya mkojo. Wahi hospitali kwa uchunguzi na
tiba.
No comments:
Post a Comment