Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Thursday, September 25, 2014

Ebola: Liberia yatoa ya moyoni kwa Umoja wa Mataifa



Monrovia, Liberia

Hivi karibuni viongozi wa Liberia wameamua kujitokeza mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuihakikishia taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa wameshindwa kuidhibiti homa ya Ebola, wakati ambapo Umoja huo umekuwa ukiahidi kuongeza juhudi za kimataifa ili kuzuia virusi hivyo.

Waziri wa Ulinzi wa Liberia, Brownie Samoukai, alitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuingilia kati, ili kuzuia ugonjwa huo wa Ebola, huku akisisitiza kuwa Ebola imekua ni tishio kwa usalama wa taifa hilo.

“Usalama wa Liberia uko hatarini kutokana na ugonjwa wa Ebola, ambao umekua ukisababisha vifo vya watu, na kuendelea kuenea katika maeneo mbalimbali ya nchi, ukiwemo mji mkuu wa Liberia, Monrovia”, alisema waziri Brownie Samoukai.

Mbali na hayo, Umoja wa Afrika AU umesema kuwa unatuma timu kadhaa za wataalam wa kutiba magharibi mwa Afrika kwa minajili ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa nchi ambazo zimeathirika zaidi na mlipuko wa homa ya Ebola zinahitaji zaidi uangalizi wa kitiba ili kuweza kukabiliana na janga hilo.

Umoja wa Afrika unataraji kutuma watu 100 ambao miongoni mwao watakuwemo madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine wa huduma za kitiba ili kuunga mkono jitihada zinazotekelezwa sasa ili kuzuia kuenea kwa homa ya Ebola.

Homa hiyo ya Ebola inaonekana kuwa na nguvu zaidi tangu ilipogundulika mwaka 1976, na imekua vigumu kuidhibiti. Homa hiyo imesababisha vifo vya watu 2296 huku watu 4293 wakiwa wameambukizwa virusi vya Ebola. Nchini Liberia pekee watu 1224 wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa Ebola, Shirika la Afya Duniani WHO, limethibitisha.

Pamoja na nchi hizo kuonekana kuathirika zaidi, lakini pia vifo vya watu saba vimeorodheshwa kutokea nchini Nigeria ikiwa ni taifa linalostawi kiuchumi barani Afrika

Sambamba na hayo, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, ambako kunaripotiwa aina nyingine ya Homa ya Ebola tofauti na ile inayoshuhudiwa Afrika ya magharibi. imeordhesha vifo vya watu 32 ambao wamefariki kutokana na Homa hiyo.



Wednesday, September 24, 2014

TABIBU!! TABIBU!!

Hizi ndizo makala na habari ambazo utakutana nazo Alhamisi hii ndani ya TABIBU
  • Fahamu namna mpapai unavyoweza kutumika kama tiba
  • Imebainika kuwa muarobaini ni kiboko ya magonjwa ya ngozi
  • Madereva waelezwa kuongoza kwa maambukizi ya UKIMWI
  • Afya za Watanzania zipo mashakani baada ya wachuuzi wa samaki kubuni mbinu mpya ya kutumia dawa za kuulia kupe kuhifadhia samaki ili wasiharibike.
  • Saratani ya ngozi inatibika

Na katika michezo pia.....


Ufahamu ugonjwa wa baridi yabisi

Dk. Geoffrey C. Lusanzu
Mpenzi msomaji wa blog ya TABIBU, hii ni makala ya kwanza katika mfululizo wa elimu ya afya juu ya kujikinga na kujitibu maradhi ya baridi yabisi (arthritis).

Baridi yabisi ni mkusanyiko wa maradhi yanayotesa watu wengi katika siku za hivi karibuni za maisha ya kisasa. Maradhi haya ni makali kiasi kwamba humtesa mtu na kumfanya kuwa mlemavu na hata kupelekea kifo wakati mwingine.

Nini husababisha maradhi haya?
Ni uwepo wa sumu nyingi za tindikali mbaya katika mwili (uric acid) na wakati mwingine ni maambukizo ya bakteria, virusi, na matatizo ya kinasaba.

Uric acid ni sumu gani?
Ni tindikali mbaya inayotengenezwa mwilini kutokana na maozea (putrid mass) ya vyakula vya nyama, mafuta ya wanyama, seli hai za mwili zilizokufa mwilini pamoja na vyakula na vinywaji vingine vingi visivyo vya asili (vyakula mtumba na vya anasa).

Inatokeaje viungo kuuma na kuvimba?Kadri ‘uric acid’ zinapotawala mwili ndivyo damu hudhoofishwa nguvu yake ya kiutendaji na misuli hushambuliwa na vipenyo vyake huziba. Hivyo ‘uric acid’ huwasha na kukereketa katika minofu sehemu ambako damu haifiki kwa kiwango kinachotakiwa. Hali ya kuvimba huwa ni matokeo ya juhudi za mwili kujihami na kujinusuru na ‘uric acid.’

Uric Acid huvamia viungo gani?

Kadri tindikali mbaya (uric acid) inavyotapakaa mwilini ndivyo mwili hujitahidi kuiondoa kwenye mkondo wa damu na hivyo kuitupa kwenye minofu au kwenye ngozi, hapo ndipo figo, ini, moyo, tezi dume, kongosho na ubongo ambapo misuli midogo ya damu katika viungo hivyo hushambuliwa na kuziba, ndipo viungo hivyo na vingine vingi hudhoofika na kuteteleka kiutendaji huku vikileta dalili za kuugua.
Orodha ya vyakula vinavyotengeneza ‘uric acid’?Orodha hii ndiyo huchangia kutengeneza ‘uric acid’ nyama za aina zote, mafuta ya wanyama , mafuta yenye lehemu (cholesterol) yaliyotengenezwa kiwandani, tumbaku, pombe za aina zote, bangi na mihadarati, kahawa, vidonge vya kemikali, vyakula vya rojorojo vya kianasa, maziwa, soda, kola na mikate mitamu iliyotengenezwa kwa hamira za kiwandani.

Naweza kutibiwa na kupona maradhi ya baridi yabisi?Kuwahi ugonjwa ni kupona, lakini kukawia kutibiwa ni kujileteleza ulemavu na pengine kifo kabisa. Hivyo ni vizuri ukawahi kupata matibabu mapema mara unapohisi dalili za ugonjwa huu.
Dawa gani zinatibu maradhi ya baridi yabisi?Dawa za kizungu (vidonge) na dawa za mitishamba (za asili) zote zinatibu kikamilifu endapo tu hazitachanganywa na kemikali mbaya, kwani kemikali mbaya inapoingia mwilini hugeuka kuwa tindikali nyingine mbaya mno ambayo huunga mkono ‘uric acid’ na vyote kwa pamoja kuuangamiza mwili taratibu pasipo utetezi.

Mgonjwa wa maradhi haya ale chakula kipi ?
Maji ni muhimu sana, hivyo mgonjwa anywe kila siku lita 2 hadi 4 za maji safi na salama. Pia ajikite kula vyakula vya asili zaidi ambavyo ni pamoja na mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali hasa yale yasiyo na sukari (citrus,) maharage ya soya pamoja nakufanya mazoezi ya viungo ya kutosha.

Ikiwa umeathirika tayari ni vizuri ukaenda hospitali au wasiliana nami kwa kupata tiba njema na kwa muda mfupi au kwa kupata nasaha.Usikose muendelezo wa makala haya sehemu ya pili!

Makala haya yameletwa kwenu na Geoffrey C. Lusanzu, ambaye ni daktari na Mkurugenzi wa kliniki ya Tiba Mbadala TANAMEREC, Kibanga, Kasulu, Kigoma. Au wasiliana nao kupitia Email: selemtiba@gmail.com. Au simu namba 0759 022 054 / 0714 284 804.

ITAENDELEA…

Tatizo la kuvimba kwa korodani




Ni ugonjwa unaoathiri korodani na kuifanya ivimbe, ugonjwa huu unaweza kusababishwa na bacteria au virusi.

Kutokana na maambukizi ya vimelea hivi bacteria na virusi huweza kupelekea kuathirika kwa korodani moja au zote mbili kwa wakati mmoja.

Lakini kabla ya kwenda mbali zaidi ni vizuri kukumbuka kwamba korodani kazi yake kubwa ni kuzalisha mbegu za kiume.

Chanzo cha tatizo hili
· Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni aina ya virusi vijulikanvyo kama ‘mups virus,’ kwa hiyo virusi hawa endapo watashambulia korodani husababisha korodani kuvimba na kupunguza utendaji kazi wake.

· Maambukizi yanayotokana na vimelea (bacteria) inawezekana ni vimelea wanaosababisha tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) na magonjwa mengine ya zinaa kama Kaswende, Kisonono.

· Kuumia kwa korodani, pengine inaweza kuwa chanzo ni ajali au michezo ya hatari, hali kama hiyo pia huweza kuchangia korodani kuvimba.

· Maambukizi ya ‘epididymis’ ni chanzo kingine cha tatizo hili, ambapo ‘epididymis’ ni mrija ambao kazi yake ni kutunza mbegu za kiume baada ya kuzalishwa kutoka kwenye korodani.
Watu walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu.
· Kama mtu hakupata chanjo ya kuzuia virusi aina ya ‘mumps’ basi mtu huyo atakuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.

· Kupata tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) mara kwa mara.

· Watu ambao hufanya mapenzi na watu tofauti tofauti mara kwa mara nao huwa katika hatari ya kupata tatizo hili.

· Kufanya mapenzi na mtu mwenye magonjwa ya zinaa

· Kama mtu alishawahi kupata magonjwa ya zinaa pia yuko kwenye hatari ya kupata tatizo hili.

Dalili za kuathirika kwa ugonjwa huu

Dalili za tatizo hilo ni pamoja na kuvimba kwa korodani moja au zote mbili, maumivu makali ya korodani, homa kali, kichefuchefu na hata kutapika na maumivu sehemu za mitoki.

Matibabu ya tatizo hili

Matibabu ya ugonjwa huu hutegema sana na chanzo cha maambukizi kati ya bacteria au virusi kwa hiyo baada ya uchunguzi kubaini nini chanzo matibabu ndipo hufuatia na yanaweza kuanzia kwa kuua vimelea vilivyosababisha tatizo hilo kwa kutumia kutumia dawa.

Athari ambazo hujitokeza endapo mgonjwa atachelewa kupata matibabu
· Kunywea kwa korodani moja au zote mbili.

· Kuwa na jipu au vijipu kwenye korodani ambalo limeathirika na maambukizi ya bacteria.

· Utasa, hii ni kutokana na kuzalishwa ‘testosterone hormone’ kwa kiwango kidogo ambayo inasaidia uzalishaji wa mbegu za kiume

· Upungufu wa nguvu za kiume.

Namna ya kuepuka ugonjwa huu.
· Wapenzi wawe na utaratibu wa kupima afya zao hususani magonjwa ya zinaa hasa kabla ya kushiriki tendo la ndoa.

· Kuzingatia matumizi ya kondomu wakati wa tendo la ndoa hususani kwa wale ambao hawajapima afya zao.

· Kupata matibabu ya uhakika pale unapogundulika una tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) au magonjwa ya zinaa.

· Endapo utakuwa na miongoni mwa dalili hapo juu ni vizuri ukawahi hospitali kupata matibabu mapema.



Makala hii imeletwa kwenu na kituo cha Victoria Therapies kilichopo Mtoni Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Au unaweza kuwasiliana nao kupitia simu namba 0658 027 027.

Endelea kufuatilia makala hizi za afya ya uzazi kwa wanaume kupitia gazeti lako la TABIBU linalopatikana mtaani kila siku ya Alhamis kwa shilingi 500/= tu

Zifahamu dalili za shambulio la moyo




Dk Fadhili Emilly

Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yeyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Ugonjwa huu upo katika orodha ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanaume na wanawake.

Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea pale ambapo sehemu ya nyama ya moyo inapoharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha.

Je tatizo hili husababishwa na nini?
Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).
Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?
Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na wale wenye umri mkubwa hususani kuanzia miaka 45 kwa wanaume na wanawake ni kuanzia miaka 55, wavutaji wa sigara, watu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zao.

Wengine walio katika hatari ni wale wenye kisukari, shinikizo la damu, walio na unene kupita kiasi (obesity), wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo zao (chronic renal failure), moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure).

Mbali na hao wengine ni wale wenye msongo wa mawazo, wanywaji wa pombe kupita kiasi, watumiaji wa madawa ya kulevya hasa ‘cocaine’ na ‘methamphetamine’ hali kadhalika na wale wenye upungufu wa vitamin B2, B6, B12 na folic acid.

Dalili za shambulizi la moyo
Dalili za tatizo hili ni maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto, kupumua kwa shida, kutoka jasho kwa wingi sana (diaphoresis), kuhisi mapigo ya moyo yanapiga haraka (palpitations), kichefuchefu na kutapika.

Sambamba na dalili hizo nyingine ni kupoteza fahamu na kuchoka haraka.

Shambulizi la moyo limehusishwa na nini?
Tafiti mbalimbali zimehusisha mambo yafuatayo na shambulizi la moyo
• Msongo wa mawazo
• Maambukizi hasa vichomi vinavyosababishwa na vimelea vya ‘chlamydophila pneumonia.’

Vipimo na uchunguzi
• ECG ni kipimo ambacho hutumika kuonesha ni sehemu gani ya moyo iliyoathirika
• Coronary angiography hiki husaidia kuangalia wapi ambapo mishipa ya damu imekuwa myembamba sana kupita kiasi (narrowing of vessels) au kuziba.
• Cardiac markers levels
• X-ray ya kifua (chest X-ray)
•Myocardial Perfusion Imaging (MPI), kipimo hiki hufanywa kwa kutumia mashine maalum ya PET Scan ambapo kinauwezo wa kugundua tatizo la shambulizi la moyo, huchunguza kikamilifu maumivu ya kifua, huangalia mwelekeo wa tiba ya kuzuia damu kuganda, hutoa mwelekeo wa ugonjwa wa shambulizi la moyo kama ni mzuri au mbaya, hutathimini ubora wa tiba ya shambulizi la moyo kabla na baada ya mgonjwa kupata tiba, huweza kutambua hata shambulizi la moyo ambalo si rahisi kugundulika kwa kutumia vipimo vingine na pia hutathimini ukubwa wa tatizo la shambulizi la moyo. Hata hivyo kwa sasa kipimo hiki hakipatikani nchini kwetu.

Ili kuweza kutambua uwepo wa tatizo hili, mwaka 1979, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka vigezo vya kutambua shambulizi la moyo. Vigezo hivyo ni pamoja na historia ya kuwa na maumivu ya kifua zaidi ya dakika 20, mabadiliko katika kipimo cha ECG, kupanda na kushuka kwa kipimo kiitwacho kitaalamu ‘cardiac biomarkers’

Matibabu
Shambulio la moyo ni tatizo linalohitaji matibabu ya dharua na lisipotibiwa kwa haraka husababisha kifo katika muda mfupi sana tangu mgonjwa apatwe na tatizo. Matibabu ya tatizo hili hujumuisha kumpa mgonjwa hewa ya oksijeni, mgonjwa hupewa vidonge vya Aspirini ndogo kuzuia damu kuganda (thrombolytic) kwa ajili ya kuyeyusha damu iliyoganda na hivyo kuzibua mirija midogo ya damu katika moyo iliyozibwa na kuganda huko kwa damu.

Vile vile mgonjwa hupewa dawa za kuweka chini ya ulimi kiitwacho ‘nitrogylycerin’ (glyceryl trinitrate) ambazo husaidia kutanua mishipa ya damu (vasodilatation), dawa mbalimbali za kutuliza maumivu kwa mfano morphine, dawa ya kuyeyusha mafuta katika mishipa ya damu kama vile ‘clopidogrel’ au upasuaji (CABG)

Njia za kuzuia shambulizi la moyo
• Kuacha kuvuta sigara
• Kufanya mazoezi mara kwa mara
• Kupunguza unywaji wa pombe
• Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.
• Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)

Aidha, kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.

Madhara ya shambulizi la moyo
• Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
• Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo (Atrial fibrillation) ambayo hatimaye hupelekea kifo.
• Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili
• Kifo cha ghafla (sudden death)

Makala haya yameletwa kwenu na The Fadhaget Sanitarium Clinic, ambao hutoa huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali kwa kutumia mimea asilia. Makao makuu yao ni Mbezi Beach Afrikana njia ya Salasala, Dar es Salaam. Au wasiliana nao kupitia 0712 705 158 / 0757 931 376
Hakikisha hupitwi na gazeti lako la TABIBU Alhamisi wiki hii kwa shilingi 500/= tu

Thursday, September 18, 2014

Mapishi pia ni miongoni mwa mambo ambayo hupatikana kupitia gazeti lako la kila Alhamisi la TABIBU. Huu ni mfano tu, lakini kwa uhondo zaidi hakikisha hupitwi na TABIBU kila wiki

Karibu tutengeneze mkate wa mbogamboga
Na Firdaws Alinus
Karibu tena mpenzi msomaji wa TABIBU, leo tunalo mapishi ya mkate wa mbogamboga. Chakula hiki tumezoea kukikuta hasa hotelini au kwenye sherehe na kwenye ndege, watu walio wengi huamini kwamba kuandaa chakula hiki nyumbani ni gharama sana. Chakula hiki kina faida kiafya katika mwili wa mwanadamu. 


Mahitaji
Mafuta ya mmea vijiko vitano
Vitunguu maji na swaum.
Pilipili mboga (hoho)
Karoti, zukini,
Kijiko kimoja cha chumvi.
Nyanya,
Hamira chenga, unga wa ngano,
Mayai 2
Sukari na maji au maziwa kikombe 1.

Jinsi ya kuandaa
Tengeneza donge la mkate kwa kuchekecha unga wa ngano pamoja na hamira, weka sukari, chumvi na mayai kisha ongeza maji na uanze kuchanganya changanya kwa kukanda kama chapati tengeneza madonge madogomadogo ns usukume donge moja kama chapati kwenye ubao na ikishakamilika kuwa kama chapati tandaza kwenye kontena ya silva yenye pembe 4 na uache kidogo kwa dakika 35 hadi 45.

Wakati unasubiri hizo dakika hizo kufika kaanga vitunguu maji na swaumu na uendelee kukaanga mpaka rangi ibadilike kuwa ya kahawia kisha weka pilipili nyanya, hoho, karoti, zukini, pasley pika kwa dakika 20 hadi 30 ikiwa tayari jaza rosti hiyo katika donge lililo tandazwa katika kontena ya silva kisha chukua donge lingine lililosukumwa kama chapatti na utandaze juu ya rosti iliyopo kwenye donge ifunge vizuri kwa madonge hayo ya ngano. 

Baada ya hatua hizo zote unaweza ukaoka kwa kutumia jiko la mkaa au oven ya umeme.

Faida za mkate wa mbogamboga.
Waisrael ni watumiaji wakubwa wa mkate wa aina hii na ni chakula ambacho hubadilisha sukari pia husaidia kufyonzwa kwa mafuta mwilini kwa sababu ya ‘chlorine’ na kuna kiasi kidogo ‘calcium’  pia huboresha neva na kuimarisha mifupa na meno pia tatizo la kutopata usingizi hudhibitiwa ukuaji wa mwili hujengwa na selenium na zink husaidia uyeyusho na kufyonza vitamin C.

Mpenzi msomaji hadi kufikia hapo tutakuwa tumehitimisha mapishi yetu ya leo, ni matumaini yangu kuwa umefurahia mapishi. Tukutane tena wiki ijayo kwa muendelezo wa mapishi. 

Kwa mawasiliano na huduma nyingine za kiafya kupima kwa computer mwili mzima, kutoa sumu mwilini, matibabu na ushauri wa chakula gani utumie na hutakiwi kutumia kulingana na afya yako. Pia kufundishwa uandaaji wa vyakula tiba fika kariakoo mtaa wa msimbazi jengo la klabu ya simba ghorofa ya tatu au piga simu namba Dar es Salaam ni 0755 093 418 na 0715 093 418 na Arusha ni 0656 540 570 na 0763 254 490. Au wasiliana nasi kupitiaa ukurasa wetu wa facebook kwa jina la febronia miracle food. Pia barua pepe ni miraclefoodfebronia@yahoo.com

Sasa TABIBU lipo mtaani kwako likiwa limesheheni makala lukuki za afya ni kwa shilingi 500/=



Hivi ndivyo komamanga linavyoweza kulinda afya yako






Dk. Febronia Kalongoti
Habari mpenzi msomaji wa blog yetu ya TABIBU, natumaini mzima wa afya. Bado tunaendelea kupeana mambo mengi mazuri ambayo pengine huyajui au unayajua kwa uchache.

Leo tunakuletea tunda la komamanga na faida zake mwilini.

Komamanga ni tunda lenye asili ya India na Persia kwa jina la kisayansi ni Punica Granatum, lakini lililetwa Marekani na wawekezaji wa Kihispania na kwa sasa limejulikana dunia nzima.

Tunda hili hustawi sana kipindi cha mwezi wa tisa na wapili, na huweza kushamiri sana katika hali ya hewa ya joto, lakini pia komamanga ni hodari katika kumudu hali ya ukame.

Kama hujawahi kula komamanga huwezi jua nini unakosa, lakini ukweli ni kwamba komamanga sio tunda tu bali ni chakula kilichojawa na afya ya vitamin, madini pamoja na virutubisho vingine vingi vinavyoweza kufanya miili yetu kuwa na afya na nguvu tele.

Tunda hili pia linajulikana kama ‘Granada’ au Tufaa la kichina (Chinese Apple), hali kadhalika tunda hili hufahamika zaidi kwa uzuri wa juisi yake,

Mkomamanga huweza kukua kwa urefu wa mita 5 hadi 8 na ina uzito wa gram 200, huku ikiwa na ‘calories’ za kutosha. Ambapo katika gram 100 komamanga huweza kutupatia kiasi cha 83 ‘calories,’ pia tunda hilo linaelezwa kutokuwa na ‘cholesterol’ wala mafuta.

Virutubisho vinavyopatika katika komamanga
Ina vitamin C kwa wingi
Vitamin B5
Vitamin A
Vitamin E
Madini kama Potassium na Iron
Mbegu zake ni chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi ‘fiber’


 

Kazi zake mwilini
Unywaji wa juisi ya mbegu za komamanga utakupa dozi kamili ya kansa, pia husaidia mtiririko wa damu kwenda vizuri katika mishipa ya damu, ambayo husaidia presha ya damu na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kiharusi.

Hulinda meno kuzuia kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu bakteria na maambukizi ya virusi ndani ya mwili, lakini pia husaidia kutibu madhaifu ya tumbo kama kuharisha, kutopata choo na maambukizi mbalimbali, matatizo sugu ya gesi tumboni hasa vidonda vya tumbo, hupunguza tindikali tumboni n.k

Matumizi
Hutumika kama tunda likiwa bichi
Hutumika kama juisi
Hutumika likiwa limepikwa.

Natumaini mpenzi msomaji utakuwa umepata kujua umuhimu wa tunda hili kiafya mwilini.

Kumbuka Miracle Food hutoa mafunzo ya kutengeneza maziwa ya soya, almond, mahindi machanga, karanga na dengu. Pia hutoa matibabu ya matatizo mbalimbali yanayosumbua mwili.

Kwa mawasiliano na huduma nyingine za kiafya na ushauri fika Kariakoo mtaa wa Msimbazi jengo la Klubu ya Simba ghorofa ya tatu au piga simu namba  0755 -093 418 na 0715 – 093 418, Facebook: febronia miracle food au Google: miracle food clinic & counseling au Email: miraclefoodfebronia@yahoo.com

Kwa makala nyingine nyingi kama hizi hakikisha, hupitwi na nakala yako ya gazeti la TABIBU kila  siku ya Alhamisi kwa shilingi 500/= tu.


Zifahamu sababu za kuwahi kufika kieleni



Ni ile hali ya mwanaume kuwahi kutoa manii wakati anashiriki tendo la ndoa, kuwahi mapema na haraka zaidi pasipo maamuzi yake au bila kukusudia.
Kwa kawaida mwanaume anatakiwa kutoa manii au kufika kileleni dakika  5 hadi  15 na endapo atafika kileleni kabla ya dakika 5 ndo tunaita ana (premature ejaculation)
Tafiti zinaonesha wanaume wengi sana wana hili tatizo na inakadiriwa kuwa kati ya wanaume 3 mmoja huwa na tatizo hili..
Sababu zinalopelekea kuwahi kufika Kileleni
  •  Magonjwa yanayoathiri tezi dume (Pro static Disorder.) Tezi dume ni kiungo kimojawapo kati ya viungo vya uzazi wa mwanaume ambayo kazi yake kubwa ni kutoa manii (semen). Bacteria wanaweza kushambulia na kusababisha ikapoteza ufanisi wa kazi yake au kupungua kwa homoni zinazoisaidia uzalishaji wa manii, kuathirika kwa hii tezi dume kunapelekea zaidi tatizo hili la kuwahi kufika kileleni (Premature ejaculation)
  •  Kujichua (masturbation), kunapelekea misuli ya uumekuwa dhaifu na akiwa dhaifu mwanaume anakua hana uwezo wa kujizuia anapokaribia kufika kileleni na kutokana na kunapelekea mishipa inayopeleka damu kwenye uume kusinyaa hivyo kupelekea damu kutofika ya kutosha kwenye uume na kufanya uume usimame legelege. Ambapo pia huweza kuwa chanzo cha tatizo hili. 3.Uharibifu wa mishipa inayotokana na utoaji wa manii, hususani mtu anapokuwa amepata ajali au kufanyiwaupasuaji(operation)
  • Msongo wa mawazo (stress), pia huweza kuathiri utendaji wa ‘hypothalamus,’ ambayo inahusika katika utoaji wa homoni ambazo zinaimarisha viungo vya uzazi. Stress inaathiri utendaji wa ‘hypothalamus,’ ambayo inahusika katika utoaji wa homoni ambazo zinaimarisha viungo vya uzazi vya mwanaume hasa uume.
  • Kuwa na wasiwasi, uoga, kutojiamini wakati wa tendo la ndoa.
  • Migogoro, matatizo ya kimahusiano. Mfano: ugomvi.
  • Kushindwa kufanya maandalizi mazuri kabla ya tendo
  • Tabia ya kurithi
  • Kuruhusu hali yoyote isiyo ya amani na utulivu itawale katika fikra zako.
  • Ulevi au kunywa pombe kupita kiasi
  • Uvutaji wa sigara, ambao hupelekea kusinyaa kwa mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume.
Matibabu
Matibabu ya tatizo hili hutegemeana namna mtu atakavyokuwa ameathirika na hutegemeana na chanzo cha kuathirika kwa kiungo hicho. Hata hivyo, kuna kanuni maalum ambazo lazima zizingatiwe katika kurudisha hali hiyo kuwa vizuri, lakini pia kuiepuka kabisa.
Unashauriwa kufika kwa wataalam wa afya endapo unasumbuliwa na tatizo hili ili kuweza kubaini ni nini chanzo cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi zaidi.

Makala nyingine nzuri na za kuelimisha kuhusu afya yako hakikisha hupitwi na gazeti la TABIBU kila Alhamis kwa shs. 500/= tu.