Dk
Mandai
Maumivu wakati wa tendo la ndoa huwakabili baadhi ya watu na
kusababisha walichukie au kukosa hamu ya kufanya tendo hilo.
Mara nyingi maumivu yanayotokea mwanzoni wakati wa tendo la
ndoa halafu yanapotea baadaye, hali hii husababishwa na upungufu wa ute
unaoilainisha njia ya uzazi na mara nyingi hutokana na maandalizi hafifu wakati
wa tendo husika.
Wakati mwingine hali hii hutokea baada ya mwanamke kumeza
dawa zinazohusisha majimaji ukeni kama vile dawa za kuzuia uzio na nyinginezo.
Adha, tatizo la maumivu wakati wa tendo la ndoa huweza
kusababishwa na athari za kisaikolojia anazokuwa nazo mwanamke. Mfano kama mwanamke
aliwahi kubakwa au kufanyiwa vitendo viovu mara nyingi mwanamke wa aina hii
huweza kuwa na hali ya kutohisi hamu ya tendo la ndoa.
Wanawake
wenye uwezekano wa kukumbwa na tatizo hili.
· Niwale
ambao muda wao wa kupata hedhi umekoma, hii ni kwa sababu baadhi ya vichocheo (homoni)
vinavyochochea kutolewa kwa majimaji ili kulainisha njia ya uzazi hupungua kwenye
damu, na wengine ni wale wenye matatizo ya maambukizi ya magonjwa katika viungo
vyao vya uzazi hususani magonjwa ya zinaa.
· Maambukizi
kwenye njia ya mkojo hasa kwenye kibofu cha mkojo huleta maumivu wakati wa
tendo la ndoa.
· Wanawake
wenye matatizo sugu ya kukosa choo wao wanauwezekano mkubwa wa kupata maumivu
haya.
· Endapo
mwanamke atafanya tendo la ndoa kipindi kifupi mara baada ya kujifungua huweza
kupata maumivu wakati wa tendo hilo. Mwanamke anapo jifungua viungo vyake vya
uzazi huchukua muda mrefu hadi kurudi katika hali yake ya kawaida, hivyo basi
anaposhiriki tendo la ndoa muda mfupi baada ya kujifungua atajisikia maumivu. Pia
tatizo hili huwapata wanawake waliojifungua kwa kuongezwa njia ya uzazi.
Wanaume huweza kupatwa maumivu ya aina hii wakati wa tendo lenyewe
au wakati wa kutoa mbegu. Pia maumivu haya husababishwa na maambukizi au
vidonda kwenye ‘gland,’ ambayo huruhusu
mbegu kutoka ‘prostate grand.’
Maumivu kwa wanaume pia husababishwa na maambukizi kwenye
ngozi inayofunika uume na magonjwa ya malengelenge na baadhi ya magonjwa ya
zinaa mara nyingi maambukizi haya husababishwa hata wakati wa kusimama. Hizo ni
baadhi ya sababu, ambazo mara kwa mara husababisha tatizo hili.
Athari
Ni jambo la muhimu kwenda hospitali unapokuwa na tatizo hili
kuliko kukaa kimya, jitahidi kumuelezea namna maumivu hayo yanavyokutokea.
Mfano utapaswa kumueleleza daktari maumivu unayoyapata yana muda gani na
hutokea baada ya tendo lenyewe au ni tofauti. Hivyo daktari atafahamu ni dawa
gani akupatie.
Magonjwa ya zinaa yanachangia tatizo hili, hivyo ni vyema
kwenda na mwenza wako mkachunguzwe na kutibiwa wote.
Tiba hufanyika kwa kutegemea sababu iliyosababishwa na
kumuona mtaalamu wa matatizo ya kisaikolojia kwa msaada zaidi, wale wenye
tatizo la kisaikolojia wanashauriwa kumuona daktari wa matatizo ya kisaikolojia
kwa msaada zaidi.
Kinga
· Ni
muhimu kuzingatia usafi kwani hupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya
maambukizo.
· Kila
mtu anatakiwa kumuandaa mwenzake wakati wa tendo hili ili kusaidia majimaji ya kulainisha njia
ya uzazi yatoke ya kutosha
· Wale
wenye njia kavu zaidi mafuta maalumu ya kulainisha hutumika, isipokuwa hakikisha hautumie Vaseline
au mafuta mengine ya mgando kwani yanaweza kurahisisha kupata maambukizo ya
magonjwa.
· Kwa
wanawake hakikisha haushiriki tendo la ndoa mara baada ya kujifungua subiri
angalau baada ya wiki sita.
Tiba
Chukua
kokwa la embe ponda ponda kausha au twanga, kisha utapata unga wake ambao utatumia
katika uji mwepesi 1x3 kwa muda wa siku 14.
Makala nyingi kama hizi unaweza kukutana nazo kupitia gazeti la TABIBU kila siku ya Alhamis kwa shilingi 500/= tu.