Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Friday, December 19, 2014

Jinsi ya kupika wali wa nazi
KARIBU mpenzi msomaji wa gazeti la TABIBU. Katika safu hii ya mapishi, leo nitawaelekeza jinsi ya kupika wali wa nazi.

Wali ni chakula kinachopendwa sana na watu wa pwani hususani wali wa nazi. Hiki ni chakula kinachopendwa sana na wakubwa na watoto.
Utagunduaje maabukizi kwenye uzazi (Diagnosis of PID)


Na Dk. Fadhily Emily
Kama tulivyokwisha katika makala zilizopita katika safu hii dalili za maambukizi kwenye viungo vya uzazi kwa mwanamke kama vile kutokwa uchafu sehemu za siri, homa, maumivu chini ya kitovu, kutokwa na hedhi bila mpangilio,
Fahamu kuhusu ugonjwa wa Kaswende - 1

Na Abdallah Juma

Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya ‘Treponema pallidum’.

Ugonjwa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi.

Ndizi na faida zake kiafya

Na Zamda Haroun

Ndizi ni tunda muhimu Afrika Mashariki na katika nchi za joto na hasa katika visiwa vya Caribbean. Mmea wake huitwa mgomba katika nchi za Afrika Mashariki.
Tunda hili ambalo lina asili ya kusini mwa Asia huonekana na rangi nzuri na mara nyingi tumezoea kuliona shambani au maeneo ya sokoni na limeonekana kuwa na faida nyingi kiafya.
Maajabu ya ‘Good Luck Plant’

Na Dk. Edger Kapagi
Mmea huu hupandwa sana na watu wengi kama maua hapa nchini Tanzania.

Mmea huu una majina mengi katika nchi za Java, Fiji, Malaysia, Indonesia, Samoa, Hawaii, Sumatra na New Guinea, nk.
Presha na Tiba Yake

Na Juma Diwani
Ama kwa hakika unapozungumzia matatizo yanayowakabili watanzania wengi bila kujali rika hutoacha kuutaja ugonjwa wa Shinikizo la juu la damu au kama lilivyozoeleaka katika masikio ya watanzania wengi ‘presha’.

Ugonjwa huu husababishwa na kuongezeka kwa msukumo wa damu katika kuta za mishipa ya damu, hali ambayo huufanya moyo kufanya kazi zaidi kuliko ilivyo kawaida ili kuweza kuzungusha damu mwilini. Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupanda na kushuka kila siku, lakini baadhi ya watu hubakia juu na hapo ndipo mtu huweza kuambiwa anashinikizo la juu la damu.

Thursday, December 18, 2014


Gazeti lako pendwa la TABIBU leo Alhamisi, Desemba, 18 mwaka huu likiwa na habari kemkem.
Pata nakala yako popote ulipo nchi nzima kwa Shilingi 500 tu.


Na kwenye michezo pata undani wa kutimuliwa Kocha wa Yanga na Je, yale maneno ya kocha mstaafu wa Manchester United kuhusu  kutambua kiwango cha timu hiyo yametimu kuelekea mwishoni mwa mwaka.


Tuesday, December 16, 2014

Dalili za tatizo la kutopata ujauzito
Tatizo la kutofanikiwa kupata ujauzito kwa mwanamke linahusiana moja kwa moja na kuwepo na tatizo kwa mwanaume.
Unaweza kusema kama una tatizo hili endapo unaishi katika mahusiano ya kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mafanikio.

Maradhi yatokanayo na nyama za wanyama
Na Dk. Geoffrey C. Lusanzu

Kwa walio wengi, ulaji wa nyama ni jambo lisiloshtua mioyo kutokana na mazoea ya ulaji wa chakula hiki.

Wengi wetu chakula cha nyama ni kitamu sana na inaweza kushangaza mno endapo utaandaa sherehe isiyokuwa na mlo wa nyama, lakini kiutaalam nyama sio chakula rafiki wa mwili wa mtu kwa kuwa ina tindikali. Mwili ni alikalaini, kwa maana hii nyama ni mpinzani wa mwili.
Je, wajua madhara ya pombe kwa afya yako?

Na Seif Oddo
Pombe ni kinywaji ambacho hutumika kama kiburudisho miongoni mwa watu walio wengi duniani kote. Wengine hutumia pombe kwa lengo la kupunguza mawazo na wapo wanaotumia pombe kwa lengo la kuondoa aibu.

Kuathirika kisaikolojia 
Na John Chikomo
1.     UTANGULIZI
Watu wengi wamekuwa wakitumia neno Matatizo ya kisaikolojia katika maisha ya kila siku wakimaanisha hali ya mtu mwenye tabia na mwenendo tofauti katika jamii. Lakini ufunguo wa kujua matukio ya matatizo ya kisaikolojia  ni hali ya mtu kuwa na msongo mkubwa wa mawazo ambayo mtu anashindwa kukabiliana nayo. Wataalam mbalimbali katika taaluma wanaelezea matatizo ya kisaikolojia katika mitazamo mbalimbali.
Ninachojaribu kukikazia katika somo hili ni kwamba mtu binafsi ndiye anayeweza kuelezea vizuri kuwa tukio lililompata limemuumiza au lah.
Tushirikiane kutokomeza UKIMWI

Na Juma Diwani
Tatizo la UKIMWI si geni masikioni mwa watu kwani huripotiwa mara kwa mara katika vyombo vya habari, tatizo ambalo husababisha vifo bila kujali rangi wala kabila huku likiongeza umaskini, idadi ya mayatima na watoto wa mitaani.


Kuvimba kwa tezi dume (Prostatitis)
Ni ile hali ya tezi dume kuathirika kutokana na vyanzo mbalimbali mfano, bakteria n. Kuathirika kwa hii tezi dume kunaweza sababisha hata utendaji kazi wake kupungua na inapatikana chini ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kuzalisha manii kwa ajili ya kurutubisha na kusafirisha mbegu za kiume kutoka kwenye korodani. Tatizo hili linawaathiri wanaume bila kujali rika lakini wanaume kuanzia miaka 50 wameonekana kuathirika zaidi na hili tatizo

Vidonda vya tumbo Kushnei
Na Juma Diwani
Haipingiki kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni miongoni mwa magonjwa yanayoisumbua jamii kwa kiwango kikubwa.

Vidonda vya tumbo ni nini
Vidonda vya tumbo (peptic ulcers) ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la chakula au katika utumbo mdogo na hivyo kusababisha ukuta wa tumbo kugusa tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali na mwishowe kupelekea vidonda.

TABIBU ALHAMISI, DESEMBA 11, 2014