Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Friday, June 24, 2016


 Upungufu wa nguvu za kiume na tiba yake 


 Na Jovin Mwingira 

MAKALA hii ya undani wa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, ilianza wiki iliyopita ambapo tuliweza tulifahamu mambo kadhaa kama vile jinsi mifumo ya mwili inavyoweza kufanikisha kusimama kwa uume na sababu zinazopelekea ukosefu wa nguvu za kiume. 

Miongoni mwa sababu tulizozizungumzia wiki iliyopita ni pamoja na magonjwa ya mishipa ya damu, mlundikano wa mafuta katika mishipa ya damu pamoja na shinikizo la damu, ambapo tuliishia tukiangalia jinsi shinikizo la damu linavyoweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. 
Tulisema shinikizo la damu la juu, huathiri mishipa ya damu ya ateri na kuifana misuli ya uume kushindwa kutanuka ili uume usimame. Pia tukasema wanaume wenye ugonjwa huo huwa na kiwango kidogo cha homoni ya testosterone ambayo huchochea misisimko. 

Aidha, lisha ya kuwa shinikizo la damu huweza kusababisha kupungua kwa nguvu kama tulivyoona pia, madawa yanayotumiwa na wagonjwa hao kuutibu ugonjwa huo pia yana athari mbaya ya kupunguza uwezo wa uume kusimama.  Miongoni mwa dawa zinazotajwa kuwa na athari hizo mbaya ni Diuretics (water pills) na beta-blockers. Duretics hupunguza nguvu za kiume kwa kupunguza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.  Pia dawa hizi hupunguza kiwango cha madini ya zinki mwilini. Mwili huitaji madini ya zinki ili kutengeneza homoni ya testosterone.  
Beta-blockers nazo huua uwezo wa neva katika kuitikia miitikio ya mwili inayopelekea kusimamam kwa uume. Pia hufanya mishipa ya damu ya ateri kushindwa kutanuka ipasavyo na kuiruhusu damu kupita katika mishipa hiyo kiurahisi. 

Ugonjwa wa kisukari 
Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume. Kusimama kwa uume kunategemea kutiririka kwa damu mwilini. 
Kisukari huathiri mishipa ya damu pamoja na usambazaji wa damu kwenye ogani muhimu mwilini kama vile moyo, ubongo, figo na uume.  Mwanaume mwenye kisukari yupo katika hatari kubwa ya kupatwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, tena katika kiwango kikubwa sana. 

Magonjwa ya figo 
Magonjwa ya figo huathiri viungo vingi muhimu katika kuufanya uume uweze kusimama na kuendelea kudumu katika kusimama.  Matizo la figo, huathiri homoni, huathiri kutiririka kwa damu kwenda kwenye mishipa ya uume. Huathiri mfumo wa mishipa ya neva pamoja na nishati ya mwili mzima.  Aidha, dawa zinazotumiwa kutibu matatizo au magonjwa ya figo, huathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume. Magonjwa ya figo, huweza kumfanya mgonjwa kutokuwa na hamu ya tendo. 

Kupiga punyeto kwa muda mrefu 
Kupiga punyeto kwa muda mrefu ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya tatizo la la ukosefu wa nguvu za kiume. Asilimia kubwa ya vijana wenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, linasababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu.  Unapopiga punyeto unakuwa unaiminya mishipa ya uume ambayo huufanya uume usimame. Matokeo yake unaifanya mishipa hiyo ilegee na ipoteze uwezo wake wa kusimama tena. Pia punyeto huweza kusababisha uwiano usio sawa wa homoni. 

Matatizo katika ubongo au mfumo wa fahamu 
Uume hauwezi kusimama bila ya kuwa na mawasiliano mazuri na ubongo. Ili mtu uume uweze kusimama, mtu lazima apate wazo la kufanya tendo la ndoa (ubongo na mfumo mzima wa fahamu unahusika hapo), akishapata wazo, ubongo hupeleka ishara kwenye mishipa ya fahamu iliyopo katika uti wa mgongo ambayo nayo hupeleka taarifa kwenye mishipa ya uume kasha uume usimama. 
Hivyo basi, ili mtu aweze kuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake ni lazima kuwa na afya njema ya ubongo na mfumo mzima fahamu kwa ujumla.  Magonjwa yanayoweza kuathiri afya ya mfumo wa fahamu yanaweza kusababisha kushindwa kusimama kwa uume.  Magonjwa hayo ni pamoja na kiharusi, kupoteza kumbukumbu na mengine mengi. Mambo mengine yanayosababisha ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na maumivu majeraha kwenye uti wa mgongo, ngiri na matatizo katika homoni.  Pia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutokana na sababu za kisaikolojia. Aidha, unywaji wa pombe, uvitaji wa sigara na matumizi ya dawa za kulevya, ni baadhi ya vichocheo vya tatizo hili. Vyakula, viungo na matunda yenye uwezo wa kutibu au kuongeza nguvu za kiume au kutoa kinga dhidi ya tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume  Vifuatavyo ni maadhi ya vyakula, matunda na viungo vyenye uwezo wa kutibu au kuongeza nguvu za kiume au kutoa kinga dhidi ya tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume:

No comments:

Post a Comment