Tabibu Tv

Tabibu Tv

EBOLA BBC NEWS

Wednesday, January 28, 2015

Hii ni Kiboko ya U.T.I

Na  Kennedy Chaya dar
UNAPOZUNGUMZIA U.T.I si jambo masikioni mwa watu wengi,lakini ukweli ni kwamba neno hilo ni kifupi cha neno Urinary Tract Infection ikiwa na maana ya maambukizi  katika njia ya mkojo,ambayo husababisha bacteria aitwaye Coli.

Mtu yeyote anaweza kupatwa na U.T.I bila kujali jinsia, rika au umri wake wake. Hata hivyo, kuna makundi ambayo kutokana na sababu za kibailojia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo.

Katika makundi hayo, wanawake ndio wamekuwa wakionekana kuathirika zaidi kuliko wanaume na hii ni kutokana na mfumo wao mzima wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria hao. Kwa kuwa mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni mfupi sana ukilinganisha na mwanaume hivyo bacteria hupata urahisi wa kuingia ndani ya mfumo wa mkojo.

Kwa  maneno mengine ni kwamba sehemu ya mkojo ya mwanamke imekuwa karibu sana sehemu ya haja kubwa na bacteria wa Colli kwa kawaida  makazi yake ni kinyeshi, hivyo wakati wa kujisafisha mwanamke ni rahisi sana kama hakuna umakini  kuweza kuchukua bacteria hao kutoka kwenye njia ya haja kubwa hadi ndogo na hivyo kupelekea  kupata U.T.I

Hata hivyo, takwimu za WHO zinaonesha asilimia 4 hadi 5 Ya wanawake wajawazito hupata maambukizi ya U.T.I.
Aidha, watoto nao ni waathirika wakubwa wa U.T.I kutokana na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia ambao unaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata tatizo hili, pia inaweza kuwa hatari zaidi kwa watoto hadi kupelekea kifo endapo bacteria hao watasambaa hadi kwenye damu na mwili mzima.

Kwa mujibu wa tafiti za taasisi ya magonjwa nchini Marekani (NKUDIC) iliyopo New York Marekani zinaonesha kuwa takribani watu milioni 8.1 duniani kote hutafuta tiba katika vituo vya afya kutokana na tatizo la U.T.I.

Madaktari wanasemaje kuhusu tatizo hilo?
TABIBU ilizungumza na Dk.Herbet Mngoma kutoka hospitali ya Shree Hindu Manal iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alisema kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea maambukizi ya ugonjwa huo ni pamoja na uchafu wa vyoo,matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha au kuoga na kufanya ngono isiyo salama.

Sababu nyingine ni kutokuwa na usafi wa nguo hususan za ndani hali kadhalika kutokunywa maji mengi mara kwa mara ambayo humpelekea mtu kupata U.T.I.


Dalili za U.T.I
Dk.Mngoma alisema moja ya dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kuhisi kukojoa mara kwa mara, mauivu au hali ya kujisikia  kuchoma choma wakati wa kukojoa, mkojo kuwa na ukungu na mara nyingine hutoa harufu kali, pamoja na maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kupata homa.

Dalili nyingine za hatari zaidi ni kukojoa damu, kupatwa na shinikizo la chini la damu,kutetemeka na kuhisi baridi.Hali kadhalika, bakteria hao wanapofika kwenye ubongo kupelekea mgonjwa kupata mtindio wa ubongo.

Madhara yatokanayo na U.T.I isipopata tiba sahihi
·     Inaweza ikasababisha maambukizi makubwa ya figo(pyenephritis) ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha.
·     Kwa wajawazito, inawezekana kuhatarisha maisha ya mama na mtoto aliye tumboni.

Jinsi ya kujikinga na U.T.I
·     Kunywa maji mengi kila siku, hii itachangia kukojoa mara kwa mara ma hivyo kutoruhusu bacteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.
·     Zingatia kukojoa kila unapohisi kufanya hivyo kwani si vizuri kuzuia mkojo.
·  
   Ni vizuri kukojoa mara tu umalizapo tendo la kujamiiana,hii husaidia kutoruhusu bacteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.
·     Kufanya ngono salama.

Kwa wanawake
·     Hakikisha unapo maliza kujisafisha sehemu za siri unaanzia sehemu ya kutolea haja ndogo ndipo usafishe sehemu ya haja kubwa.Hii itakuepusha kupata bacteria walio eneo La haja kubwa kuingia njia ya mkojo.
·    
Epuka kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu, kwani husababisha kuua bacteria rafiki wa ukeni.Kwa kufanya hivyo, utakaribisha bacteria wa U.T.I kuzaliana kwa wingi. Vilevile, Dk.Mngoma alisema kuwa ugonjwa huo unatibika na alizitaja baadhi ya dawa ambazo hutibu tatizo hili kuwa ni amoxicillin, erythromycin n.k. Hata hivyo, daktari alisisitiza kuwa ni vizuri kuzitumia dawa hizo baada ya kufuata ushauri wa madaktari.

Wataalam wa tiba asili asemaje?
Gazeti hili lilimtafuta mtaalam wa tiba asili, Dk. Majaliwa Ibrahimu kutoka katika kituo cha Mkunazi Herbalist Clinic kilichopo Kigogo jjini Dar es salaam. Daktari huyu alisema kuwa dawa ya asilia inayotibu tatizo hilo ipo na inaitwa  UHT-POWDER  ambayo humsaidia mgonjwa kupona kabisa  na  kutomrejea tena  tatizo hilo, alisema.

Kwa mujibu wa mtabibu huyo alisema dawa yake hiyo ya miti shamba imekuwa msada mkubwa kwa UTI sugu  wengi   waliotumia husasani wanawake na watoto walinufaika nayo.

Mtaalam wa tiba asili kutoka uturuki anasemaje?
Aidha,kwa mujibu wa utafiti wa Dk.Oz ambaye ni raia wa uturuki anasema kuwa hakuna sababu ya kwenda kumuona daktari unapohisi dalili za U.T.I, badala yake unaweza ukajitibu mwenyewe  ukiwa nyumbani.

Unachotakiwa kufanya ni kuchukua hamira kiasi cha robo kijiko cha chai changanya na maji safi na salama glasi moja kisha kunywa mchanganyiko huo.

Kwa kufanya hivyo, utasaidia kutengeneza magadi mwilini amabyo huzuia bacteria wengine wa U.T.I kutozaliwa.

Wananchi wanasemaje kuhusu ugonjwa huu
Kati ya watu 20 waliofanya mahojiano maalum na gazeti hili walionekana kuwa na uelewa kuhusu ugonjwa huu,ingawaje wanawake wengi walionekana kukiri kukabiliwa na tatizo hilo.

Pamoja na hayo, waliiomba serikali kupitia wizara ya afya kutoa elimu zaidi juu ya tatizo hili, jambo ambalo litawaongezea uelewa juu ya ugonjwa huu.


3 comments:

  1. Hiyo Hamira unakunywa kwa muda gani mm ninayo hasa nimepima kabiss hospital

    ReplyDelete
  2. Dr kanyas mtaalamu wa tiba asili anazo dawa za nguvu za kiume ..za kurefusha uume na kunenepesha uume .anatibu UTi sugu..
    Ugumba....maji machaf ukeni harufu mbaya ukeni ..mtafute dr kupitia 0764839091

    ReplyDelete
  3. ndugu @stephano huyo dr anatibu kweli tatizo la nguvu za kiume au ndo walewale coz mm ninashida hiyo ila sasa wengi wao wananiibia tu pesa na wengine wananipa dawa za siku mbili tatu na zikiisha tu hali inarudi awali






    ReplyDelete